Sehemu Ya Tano (5)
Wajumbe wote: wakakumbuka, wakauliza sasa hii inahusiana nini na waume za watu?!
Mjumbe no 5: kama wake za watu wanalalamika ndoa haziendi, hii ni opportunity kwetu sisi akina single ladies.
kwani sisi tunataka nini, si mume wa kukupenda na kukupa mapenzi, badala ya waume kukitembeza kila mahali, bora sisi tuwasaidie wake zao. Bora wanaume wawe na sehemu 2 za kwenda, mwisho wa siku tutakuwa tumejua jinsi ya kuishi na wanaume na soon tutakuwa na nyumba zetu na waume wetu!https://pseudepigraphas.blogspot.com/
Wajumbe wote: aaah hamnaa, hio laana, we mpare acha ushenzi kabisa hatutaki laana hapa leta idea nyingine mama!
Mjumbe no 5: nyie sikilizeni, ndoa ambayo imekufa inamfanya mwanaume atafute pa kupumulia, pa kupumzika, sasa nyie mnashida gani mkifanyika mapumziko ya waume za watu? kwani mnahamishwa nyumbani? si mnakutana hotelini? mambo yakitiki ukahama nyumbani akataka kuoa inakuwa bahati yako.
Wajumbe wote: wakanyamaza kimya wakasikiliza kwa makini sasa!
Mjumbe no 5: mimi nawajua wadada wamoja, akaanza kutoa hapo ushuhuda wa wale waliofanikiwa kuiba waume za watu wakaolewa wao, wakiwa na miaka 40 na mpaka sasa wamezeeka wote wakiwa na miaka 60
Wajumbe wote: wakanyamaza kimya, wanaskiliza kwa makini mpango mkakati wa mjumbe wa 5
Mjumbe wa 5: sasa ndo hivyo kwa anaetaka kuingia kwenye hili game aseme, ni kwa ajili ya kuwasoma hao wanaume na kwanini hatuolewi basi, ikifika sehemu ukakoleza penzi wanaume akachizika akakuoa basi bahati yako ila hii ni research, tunaenda kwa kujifunza
Wajumbe wote: lakini hii tabia ya kuiba waume wa watu ni mbaya sana, je hao watoto wao wakipata shida hawahudumiwi vizuri kisa wewe unakula raha ina faida gani?
Kwanini tusiwapate wale ambao wameachana au wale wajane wapo kibao tukajifunze huko lakini sio waume za watu?
Mjumbe no 5: ivi unajua moto wa kutembea na mjane, kila siku atakuwa anakuliza kwa kukufananisha na marehemu mke wake, mpaka aje asahau msiba wa mkewe amtoe kichwani mama yangu ushaumia sana, hatokupenda atakuwa anakumega huku akikwambia namkumbuka mke wangu alikuwa mzuri sana akiwa hivi na vile
haya tukirudi kwa mwanaume alie mtalaka, ataishia kukumega akuache, maana mpaka kapata talaka, ina maana yupo huru kwa muda mreeefu sana, na atakuwa na hasira zake kibao juu ya wanawake, hapo sasa ukikaa utaisoma namba
Wajumbe wote: sasa tunawapataje hao waume wawatu, hatutaki waume njaa lakini,
Mjumbe wa 5: akawatajia wababa wenye hela mjini ambao ndoa zao zipo juu ya mawe, wenzake wanashangaa huyu mjumbe amepataje kuwajua hawa?
Akawaeleza sehemu wanaishi, Baa wanazoenda, vitu wanavyopenda, familia zao zinapoishi, nyumba wanazoishi, kazi wanapofanya, yani ni mambo makubwaa wanaelezwa
Wajumbe wote: wakaanza kuwa na wasiwasi na mjumbe no 5 kuwa kama yupo sawa?!
Mwisho wa maelezo yote, akaanza kuwagawa vibopa kwa kila mjumbe kasoro yeye, wakawa wanashangaa, wakamwuliza je wewe umempataje wako
Mjumbe no 5: mimi wangu alikuwa ananisumbua sana akija ofisini benki, nikaamzungusha ila katika kufikiria fikiria kwangu nikaamua kumsikiliza, nawaambia huu ni mwezi wa 3 nipo na yule bwana, mkewe hajui, naishi kwangu anakuja weekend anashinda masaa 12 anarudi kulala kwa mkewe, sasa hivi najua kwanini na wapi wake za watu wanapoharibu, ila siwezi kuwahukumu kabisa wake zao maana majukumu ni mengi na najua hata mimi akikaa nami kwa muda mrefu atanichoka ataondoka atafute kwa mwengine mdogo zaidi yangu amdanganye amchezee amuache...
Nilichoamua kufanya ni kufunga moyo wangu kwa huyo mume wa mtu, nafanya mahusiano nikiwa nimefunga moyo na roho kabisaa, si nipo kwenye reseach ikiisha nambwaga, kwani kuna nini cha maaana ananipa ambacho sina, mimi sio security yake wala nini!
hii miezi 3 nimejifunza mengi sana na namwamini Mungu nitaolewa na nitakuwa na familia yangu!
Wajumbe wote: kiru! je ukipata watoto nae? utafanyaje? maana ajali ni kazini mama!
Mjumbe no 5: kwani single mothers hawaolewi? Wake zao wanavyowa misstreat waume zao na kujitamba kuwa ndio securuity yao kubwa hawajui sisi wa-nje tunavyowashangaaga tu!
Wake zao wakisema mwanaume huyu wa nini, kuna mtu mwengine anajiuliza nitampata lini!
Hio ndio opportunity cost my dears! changamkeni mmekaliza makalio mnalalamika lalamika tu, mnataka Yesu aje awape mabwana mtasubiri sana!
Masaa yanagonga tuna 35 hatuna hata watoto hapa ni kujichatua ufahamu na akili mpaka kieleweke; na hao wake za watu wajifunze kutunza waume zao kwa unyenyekevu sasa ni fundisho kwa wote my dears!https://pseudepigraphas.blogspot.com/
huyu wangu hanisumbui unajua hanisumbui, na nilichokuwa nakikosa kwa ex boyfriend wangu ninakipata kwa huyu maradufu, hata kama halali kwangu lakini ni opportunity ya mimi kupata anaenipenda mbeleni
Wajumbe wote: sasa ukija kukamatwa na mkewe?
Mjumbe no 5: utakuwa ni boya, wewe mke wake unamfuata wa kazi gani labda? unataka nini kwa mkewe? mashindano au ukichaa?
kwani mumewe alivyokutaka alikuja kukutaka na mkewe au?
Huyo mkewe wewe wa kazi gani labda? unamikakati nae kivipi?
Hayawahusu hayo yao na yako ni yako! wewe fanya yako to the fullest achana na mke wake
ikatokea kweli mke wa mtu kakufumania lazima ujibadilishe rangi, jifunze kuichangamsha akili yako, mwizi hata siku 1 akikamatwa hakubali kuwa mwizi na wewe usikubalki kukamatwa kiboya boya, hama mtaa, mji, wilaya, mkoa, Dar es salaam ni kubwa sasa mpaka kibaha mpaka Bagamoyo hamia!
kha!
Wajumbe wote: wakawa wanamshangaa mjumbe no 5 kuwa ni mzima kichwani au?
Jomana: kwahiyo bindada mishen yako yaisha lini? na huyu bwana naanzaje kumtext?
Nampataje? embu tupe mbinu
Mjumbe no 5: akawapa mbinu zote alizotumia yeye wenzake wakamkubali kuwa ni noumer, akawaomba wanunue simu tochi kwa ajili ya kuwasiliana na hao side husband, wa register namba zao za simu kwa majina ya kiume sio ya kike ili kugundulika iwe ngumu,
Wajumbe wenzake wakaguna wengine wakakataa wengine kama mjumbe no 2 na jomana wakakubali ila Pendo alikataa katu katu akaachiwa namba na maelekezo ya kibopa wake!
Waliporudi Bara, wenzake wakafanya yao wakafanikiwa kasoro Pendo, Mjumbe no 5 alipoona pendo anazubaa zubaa, akaamua kununua simu na namba feki, akaanza kumwendea huyo kibopa, kinyume na Pendo, wakawa wanachat kimahaba, Kibopa akaomba waonane, akawa anamzungusha akamzungushaa, mpaka akakubali akaamua kumfuata Pendo na kumweleza ukweli, haya mama simu hio hapo jina la simu limesajiliwa kwa jina la Patric, anataka muonane Jollies Club leo ijumaa, nenda mama kamsikilize, akampa mpango mzima na jinsi ya kuongea nae kama yeye alivyokuwa anaongea nae, Pendo anashangaa tu heee hii ya leo kali, Mjumbe no 5 akamsihi sana aende akajifunze kitu sio lazima alale nae, Pendo akamkubalia poa naenda kesho nitakupigia
Ndio mwanzo wa Pendo Mmachame kuonekana maeneo ya Isumba Lounge, akiwa na Kibopa!
Maongezi maongezi Kibopa akakoleaa!
Kibopa: totoz zuri, tototz laini, totoz umeumbika, totoz nimekupenda unavyonifariji , totoz natamani sasa hivi niende nikakubatize nikuone unavyofanana
Pendo: akawa anacheka ndani kwa ndani anatamani kupasuka kwa kicheko lakini anajikaza, akawa anabaki ana smile, mara atukane kimoyomoyo mjumbe no 5 mshenzi kabisa, yani ananiuza kwa waume za watu aya bwana!
Maongezi maongezi na pombe kali za kutosha, Pendo kucheki muda ni saa 6 usiku, hajawahi kuingia kwao saa 6 akaona hapa ishakuwa msala, akampigia Mjumbe no 5, mama naja lala kwako siwezi rudi kwa mchaga nitakufa kabla sijaingia nyumbani!
Mjumbe no 5: akakubali maana kesho yake ni jumamosi, sawa mama wewe kula nchi ukimaliza njoo kwangu milango na madirisha yote yapo wazi
Usiku huo huo Kibopa akamchukua Pendo mpaka guest house, shughuli shughuli na wewe, Moven Pick moujaaaaaa!
Pendo Binti bikira wa miaka 35 ameenda kuchinjwa na Kibopa!
Shikamoo waume za watu!
kiru, ndoooroooooboooe! ngoja nikanunue gazeti nijipepeeee!
SEHEMU YA 2?
?
A. BAA TUKIO BAYA BALAA?
Wajeda wakazama Moven pick, Kibopa akachukua chumba cha presidential Suite, totoz Pendo aliemchanganya Zee la watu kwa mahaba akatundikwa kwenye presidential suit!
Kwa wale ambao hamjawahi kuingia kwenye vyumba vya Presidential Suite ni habari nyingine, usikubali kufa bila kulala kwenye hicho kitanda, kwanza huduma yake yenyewe ni noumeeer!
Kibopa anajua leo nakula show ya maana, show ya kimalaya kumbe amebebana na bikra! ukisikia Mbuzi kwenye kisahani ndio hii
Ahahahahaha
kufika kwenye show anashangaa mrembo amekaa kama gogo, akahisi labda mrembo ana mzoom kwanza show yake ya kizee, Kibopa akafanya yake aliojaliwa ya experience ya miaka sitini na zake! alipojaribu kwenda kuvua samaki anashangaa mrembo anakimbia mara anasema unaniumiza kwa kuning'ata,
Kibopa akashtuka akaona labda ni pombe, kadri alipozidi kuendelea na mahaba yake demu analalamika, Kibopa akachoka, maana jitihada zote na mautamu ya awali aliyojaribu kumfanyia Totoz, totoz hakuonyesha ushirikiano.
Na hivi ni mtu mzima wa miaka 65 akawa anahisi anachezewa akili, ikabidi amwulize Mama shida ipo wapi? mbona huduma ya simu imezidi ya live? ikabidi binti wa watu ajiseme, oh! unajua mimi sijawahi kabisa kucheza michezo ya wakubwa, leo ndio mara yangu ya kwanza, naomba unihurumie mzazi uende na mimi mdogo mdogo,
Dah! Kibopa akiangalia ameangusha madolari pale mapokezi, akaona isiwe shida, ingekuwa hotel ya elfu 50 angeondoka lakini sio kwa zile dola alizozitupa akaona aende nae mdogo mdgo mpaka kieleweke!
ikabidi ampooze kwanza kisaikolojia kwa kauli, kumpeti peti na nini akatumia karibia dk 15, Pendo haelewi yupo defensive na kujihami utadhani yupo vitani au anacheza mieleka, anatoa macho kama mjusi kabanwa na mlango... ahahahaha
Kibopa ivyo ivyo kibishi akaenda nae mdogo mdogo, kweli totoz akaanza kuonyesha ushirikiano, speed ya treni ikaongezeka, mara 30, mara 45, mara 55 mara 100 mara 120 kuja kuibuka ameshavuka ukanda wa gaza, Pendo analia kama kinanda cha kanisaa, haaaaaaaaleluyaaaa, haaaaaleluyaaa naumiiiiaaa naumiaaa nauuuuumiiiiaaaaaa!
Ndio ushangae binti wa miaka 35 analia kama mtoto mdogo, aibuuuu, hii ndio shida ya wadada wa kimachame, nje wanaonekanaga wajanja kitandani hamna kitu!
Mzee kaskiliza makelele mpaka kachokaaa! si unajua mababu ambavyo hawapendi kelele, akaamua kuondoka usiku ule ule baada ya kumkamua na kukata mnyororo wa Pendo, kamuacha Pendo analia hataki kusikia la mkuu, chezea Bikra ya miaka 35 wewe!
Pendo kuja kutulia na kucheki saa kumbe ni saa 8 usiku, akaona ampigie Mjumbe no 5,
Simu: ikaita weeeee, baada ya dk 10 ikapokelewa, Best nafaaaa tafadhali njoo Moven Pic Presidential Suite
hapa sina hata 100 nahisi tutadaiwa na huyu mzee kanichezea faulo ya kufa mtu,
Baada ya nusu saa Mjumbe no 5 akatia timu kwa hotel, kufika anamkuta Pendo amevimba macho kwa kulia akiangalia kitandani midamu kama wamechinja ng'ombe,
Mjumbe no 5: heee we pendo, umemuua mzee wa watu au? yupo wapi Kibopa?
Pendo: hapana ndio maana nimekuita leo nimekuaibisha hakuna tena, ivi unajua mimi nilikuwa bikra?!
Mjumbe no 5: Bikra?! ikabidi akae kwanza kwenye kiti sio kwa ule mshituko, wewe Pendo ni bikra? doh! siku zote hizi Pendo wewe kumbe sio mwenzetu? lakini mbona hauonyeshi? mbona mjanja mjanja sana, haki Pendo huyu mzee hatorudi tena kwako nakwambia,
uuuwi tena umekosa bahati maana ameachana na mkewe mwezi uliopita mahakamani,
uuuwi Pendo huyu baba anahela vibaya mno!
Nakufanyaje rafiki yangu yani kama ni darasa kwako nakurudisha elimu ya awali au chekechea katika mahaba!https://pseudepigraphas.blogspot.com/
Lakini, embu ngoja akashuka chini akakaaa kakam dk 10 akarudi haya Pendo ngoja wafanye usafi kwanza, hapo saa 9 nanusu usiku, wakasubiri mpaka usafi usishe na mashuka kubadilishwa ikabidi walale pale pale, asbh wakaoda breakfast kwanza wakaoga na kuchezea maji na kupiga ma selfie ndio wakaondoka maana chumba kililipiwa mpaka saa 5 asubuhi.
Wakiwa wanakunywa chai Mjumbe no 5 anamtania Pendo, shoga bikra yako ni 1st class maana inatolewa kwenye presidential suit kama hii? eh wewe ni noumer umshukuru Mungu, wengine Bikra zetu zilitolewaga migombani kwenye michongoma, mchongoma chini, nanilihii katikati, umeshikilia mgomba pembeni, unachomwa chini, unachomwa na kwengine hatari! maumivu mara 3, sitaki hata kukumbuka iyo siku asee ila sikudanganyi mpaka leo i wish ningekuwaga bikra, ungenieleza hali yako mapema mpenzi wala nisingekuponza, tatizo na wewe msiri sana wewe mmachame!
Pendo: akawa anasmile tu, asante shoga kidawa kwa kunitia moyo
Mjumbe no 5: usijali, mimi nipo kwa ajili yako, pole kwa yaliokukuta wala usijiskie vibaya, ila shogari itabidi nikutafutie kungwi, aibu ulionipa mwisho leo, yani kwanza hapa sipati picha jinsi gani ulivyokuwa unachemsha kwenye show, mzee wa watu anaenda kushoto, wewe unaenda kulia basi tu ilimradi, iyo kama ni mziki unaitwa mziki wa shule ya jumapili (Sunday School), mwingine anapiga kinanda mwingine ngoma mwingine filimbi basi ni tafaruku hakuna kusikilizana kila mtu na lake ilimradi show imechezwa, ahahahahaha pole Pendoooo! uuuuwiiii chezea Presidential suites wewe, utatoa utoiii!
Walipofika kwa Mjumbe no 5 Pendo bado analia, Mjumbe akamkemea usinichoshe na wewe nani alikwambia ujitunze mpaka sasa hivi? ningejua wewe ni bikra ningekupa vijana wangu kwanza wakupagawishe ndio nikuingize kwenye kazi kama hizi za show za kibabe.
Wewe kaa hapa, mpigie mzazi wako mwambie umesafiri upo kizazi Arusha, ulibeba nguo asubuhi, ongea na mama yako mwambie utarudi baada ya wiki 3, sawa? alafu utakuwa unaishi kwangu mpaka ukomae kwanza maana ukirudi tu watakujua, wazazi wanajuaga kwa kuangalia tu, wale watu ni hatari sana kama wachawi falni hivi!
Basi Pendo akafuata masharti ya mjumbe no 5 akaongea na mama yake Mama akamuelewa sawa mwanangu kazi njema,
Jumamosi hio kukawa kimya, yule Kibopa hakutuma cha sms wala kupiga simu,
J2 kimya, Pendo akajua hapa nimevamia gari kwa mbele nimeshaumia nikubaliane na hali halisi
J3 akadamka na mjumbe no 5 kwenda ofisini, ofisi anaiona chungu, kila mteja anaekuja mtu mzima akawa anahisi ni Kibopa kumbe sio, ikaenda hiyo hali kwa muda wa wiki 2 mpaka akazoea akakaa sawa!
WACHAGA NA POMBE:
Baba yake Pendo alionekana Bar na marafikizake wanakunywa pombe, si unajua wazee wa kichaga na pombe! piga ua iyo ndio raha yao kuiacha ni ngumu labda wawe wameokoka!
kama kawaida yao wakiwa Bar wanaongea kwa nguuuvu sana na hivi walishazoeleka na mwenye bar huwa hana shida nao.
Wanapata mastori ya mjini, mambo ya siasa mambo ya mpira mambo ya habari na mambo yao ya zilipendwa, si unajua tena wastaafu wakikaa pamoja wanavyojikumbushia
Kwenye hiyo Baa walikuwepo Baba yake Jomana na Omana (Wapare), Baba yake Pendo na Manka (Wachaga), na wazee wengine 3 jumla walikuwa watano
katika maongezi yao ya kiutu uzima, wazee watatu, wakawa wanajigamba kuwa wanatembea na madogodogo watoto wa mjini, mabinti wadogo mabinti watamu, mabinti wa ukweli, wanatoa show zote za kifalme, show za kujichetua, show za kimalaya, ambazo wake zao wanaona kinyaa kuwapa
wakawa wanajigamba pesa wanazowapa mwingine anasema nimemnunulia nyumba baada ya miaka 3 ya mahusiano, mwingine nimempa gari, mwingine nimempangia mikocheni, mwingine nimemnunulia kigari na kiwanja, mwingine nimemsomesha, mwingine akasema kanizalia mtoto, mwingine amezaliwa watoto basi wanaona raaaahaaa kujifanya vidume kumbe washenzi tu.
Baba yake Pendo akawa anakemea vikali kuhusu michepuko, mtakufa na miwaya wazee wenzangu, kwanini msikae na kutulia na wake zenu mle penshen zenu vizuri mnatupa hela kwanini lakini mnaharibu maisha?
Wazee wenzake wanamcheka, we mshamba kweli, embu jinyakulie chata ya uzeeni unakuwa mpole namna hii maisha yenyewe mafupi muda wowote unarudisha namba kwa Muumba
Baba yake Omana akawa anasikiliza kwa makini, yupo neutral hachagui upande wa kuegemea si unajua mzee aliefilisika atajinyakuliaje mchepuko? wakati analishwa na wanae wanaofanya kazi benki
Wazee wenzake walikuwa na convincing power kubwa juu ya michepuko, ikabidi Baba yake Pendo aingilie kati na kuuliza swala zima la michepuko linaendaje, akapewa ramani yote na jinsi ya kuwapata, "ni lazima apate kimwana anaemzidi kifedha ili amshikishe adabu na kumtuliza" wakasema.
"Piga nae round kama mara 10 mchore kama ni gold digger au nini usimpe kwanza hela, msome hata miezi 6 mpaka mwaka, uwe anampa nauli za bajaj na taxi kwa kumficha asionekane, sio dalaldala, maana huko kwenye daladala anaweza pata kijana mwenzake au akishuka kwenye daladala akapata kijana akampagawisha akakukimbia" Akaongea mzee wa 2.
Baba Omana: Mimi naona michepuko haitonisaidia maana nimefilisika, nitampa nini?
Kibopa: Tena kweli umenikumbusha, kuna sehemu wanahitaji Hotel Manager hapa hapa Dar, naomba uende kesho nimeku refer. Kesho saa 3 juu ya alama uende pale akamtajia jina la hotel, utakutana na mtu fulani (akamtajia na jina akamwandikia na namba ya simu kama hatomkuta) ajitahidi awahi kufika kabla ya muda, nende utapata kazi maana una experience hio.
Basi baba yake na Omana akafuraaahi kesho anaanza kazi, akanywa pombe yake kwa furaha huku kibopa anamuagizia nyingine 3, kumpa pongezi.https://pseudepigraphas.blogspot.com/
Baba Pendo: unajua sisi wachaga kazi yetu ni kusaidiana, alichokifanya Kibopa ni sawa kabisa, ameonyesha tabia ya kichaga ingawa yeye sio, ndio tabia halisi ya uchagani sijui wapare kama mnasaidianaga!
Hamna haja ya kumwona mwenzio anahangaika alafu pombe tunakunywa wote kumbe kuna mtu anaumia sio vizuri kabisa, ulivyofanya hivyo mzee wenzangu nakupongeza sana, asante sana kumsaidia baba Jomana.
Kibopa: We Mzee bwana, acha maneno mengi, kusaidiana hailetwi na ukabila ni mtu alivyo na jinsi alivyolelewa
Anyway, tuachane na hayo nataka niwaambie wazee wenzangu, kuna kimwana nimekipata juzi kati, dah sikuamini, mrembo alinipagawisha kwenye simu kweli kweli, nikapagawa sana, nikimpigia simu anaongea kwa sauti ya mahaba kabisa, tukawasiliana kama wiki 3 nikaomba kuonana nae akakubali.
Tulipokuja kuonana, kweli sauti na maongezi yake na mwili wake vinaendana havipishani hata kwa nukta!
totoz ni mzurijeee, anateleza ukimshika kama mlenda, ndio ni kama mwanangu wa kumzaa ila mtoto ni mzuri balaa, basi tukachukua chumba pale Moven Pick, nikamchukulia Presidential Suite tukazama kwenye mahaba, huenzi amini wazee wenzangu sikuamini nilichokikuta katikati ya mechi
Wazee wenzake: enheee! ulikutana na nini? au alikuwa jini? ahahahahahaha huku wanamcheka! mzee umeumbuka naona ulifikia 40 yako usiku huo ahahahahahahahahaa.
Kibopa: nimekutana na miujiza ya mwenyezi Mungu, hauwezi amini nimemkuta binti mwenyewe ni bikra!
Wazee wenzake: wakamchekaaaaa ahahahahahahahaha! uuuwi mbusi kwa kunia iyooo! wakachekaaaa, ila baba yake Pendo hakucheka, akawaangaliaaa alafu akamwangalia na Kibopa akawauliza, kwani kuna shida gani kupata bikra?
Wazee wenzake: ah! bikra hatuna muda nayo, tunataka vitu vilivyokuwa na experience, vinakuchangamsha kiakili na kimwili, mambo ya kuanza kuchinja mbusi na mbusi ya ukubwani ilivyo ngumu hizo nguvu sisi tunapata wapi? hizi Bikira unaachia vijana wenye nguvu zao, sasa kwa mfano mzee wetu hapa angemtoa bikira yule binti akafa au akazimia unadhani ingekuwaje si ni polisi kesi hio tayari?
Baba Pendo: mimi nadhani ungeshukuru Mungu pamoja na watoto wa mjini kutotulia na kuwa mapepe, wengi wao wamebeba ukimwi. Sasa Kibopa umepata bikra unapoteza bahati?
kweli wewe hauna maana kabisa
Wazee wenzake: wakanyamaza kimya wakawa wanamsikiliza Baba Pendo
Baba Pendo: mimi ningempata huyo bikra ningemshikilia mpaka mwisho pamoja na umaskini wangu, maana huyo hana mambo mengi, mimi ndio ningemfundisha mapenzi yote ili hata angekutana na vijana lazima angekumbuka mti wake wa awali ambae ni mimi.
Ila kila mtu ana mtizamo wake, na hivi mzee mwenzangu umempa mkeo talaka, ungemweka ndani huyu binti kabisaa maana ni mtoto toka Mbinguni, hajajichafua, hajachezewa kabisa yani ni kama kununua gari jipya linalosoma km 0, sasa nyie siwaelewi mnang'ang'ania km laki 1 ukiendesha kidogo limekongoroka unakimbia gereji kulipigapiga unapoteza hela chungumzika kufufua kitu kilicho expire.
Haya ni maoni yangu mimi lakini, kama haumpendi naomba niletee mimi basi nihangaike nae na umaskini mwangu
Kibopa: weeee! thubutuuu!
unajua unachokiongea Baba Pendo ni kweli kabisa huku anakunywa wine yake ya Hennessy, kweli mzee mwenzangu, hata hivyo nimeshachoka na haya maisha ya kufukuzia vibinti vidogo, ngoja niangalie kama nitaweza kutulia na huyu binti wa juzi, akinizingua namtupa chini.
Baba Omana: akamwangalia Kibopa akatikisa kichwa, baadae akamwuliza kweli utatulia wewe mzee wa kipare? maana wapare bwana doh
Kibopa: wapare wana nini tena? we niache bwana!
Baba Pendo: hivi mzee mwenzangu ilikuwaje ukaachana na mkeo? kulitokea nini?
Kibopa: ah tuachane na hayo, ndoa iliishaga muda sana basi nilikaa tu kwa ajili ya watoto, watoto sasa wameolewa nikasubiria Anniversary ya miaka 40 ya ndoa nikawaita watoto waliokuwa Uingereza, nikawaeleza nampa talaka mama yenu nimemchoka na matatizo yake, nikampa talaka siku hio hio nikamuachia nyumba kubwa mimi nikaenda kukaa kwenye nyumba ndogo niliyoijenga Tegeta
Watoto walimind sana lakini watafanyaje hayo ni maamuzi yangu mimi, na sasa mwaka umeshaisha kila mtu anaishi maisha yake, mimi nipo kivyangu na totoz wa mjini nabadilisha tu mashuka, nikiskia kiu najua wapi nitakunywa maji, ila maji nimekunywa sana, lakini kiu hakikatiki
Baba Omana: kwanini usirudi kwa mkeo tu
Kibopa: hapana sirudi hata kwa bure, yule ameshapata bwana mwingine huko kanisani, wanaimba wote kwaya kuu sijui kwaya ya wazee, na yule bwana alivyo hupenda mteremko sasa hivi ameshahamia pale nyumbani kabisaa, kwaiyo mimi naishi maisha yangu kwa sasa
Wazee wenzake: wanashangaa, wanamhurumia mzee kama yule anavyohangaika kama mbwa aliekosa makazi, aibuuu!
Baba Omana: basi hakuna kilichoharibika mzazi huenda Mungu amekuletea huyo bikira wewe tulia nae kama vipi!
Baba Pendo: kama haumtaki bikira nimeshasema naomba uniletee mimi nitaenda nae mdogo mdogo najua bikira bado haijatoka yote, lazima kuna mabaki na nyuzi na minyororo haujaikata, ahahahahaha
hauwezi ukawa umemvunja bikra yote kwa masaa 4 sio kweli, wewe nisogezee mdoli huyo nimlee!
Kibopa: tatizo lako Baba Pendo una tamaa sana, kujidai dai kama umeokoka kumbe hauna lolote, wewe juzi kati nimekuona kinondoni unatoka gesti na kimama kimoja kichafu chafu. kweli mke wako ana kazi sana nawewe
Lakini nashukuru umelileta mwenyewe hili, sikunyingi nimetaka kuongea na wewe jinsi unavyowalea na kuwanyanyasa watoto wako
Unajua huyu baba watoto wake hawana sauti, mkewe hana kauli kwake kabisa unaweka mazingira ya kiboya ya kifalme kwa familia yako ili iweje sasa?!
Mimi kila nikikuangalia nakuona hauna raha unaishi maisha yako kama gari bovu tu! hauna lolote,
Leo hii mimi nikupe bikra ukamchakaze kama ulivyomchakaza mkeo, kwanza mke wako yupo kama house girl amedumaa na kukomaa kama anafanya kazi moshi shambani! hana tofauti na wamama wa kijijini huoni hata aibu?!
Wazee wenzake: wakaanza kumtuliza Kibopa, basi bwana achana na haya maneno hayakuhusu
Kibopa: ndio maana watoto wako hawaolewi maana wanachukia wanaume kwasababu haujawapa mapenzi ya ubaba kwa karibu na mimi nakwambia ukiendelea hivyo watoto wako hawatoolewa ng'o. umemtesa sana yule mama namwonea huruma kwanza nikiskia yule mama amekuacha nitampa hata milioni 100, sio kwa mateso yale, wewe mzee hauna hata huruma kabisa na watoto wako wala mke wako!
https://pseudepigraphas.blogspot.com/
watoto wako wataishia kuzaa tu na waume za watu, utaletewa wajukuu waliozaliwa nje ya ndoa kwasababu unavuna ulichokipanda ndugu yangu, mbona sisi watoto wetu wameolewa vizuri kwa ndoa na tuna wajukuu waliozaliwa ndani ya ndoa hata kama tumeharibu uzeeeni inaeleweka wewe umewaharibu wale watoto tangu utotoni
umepata hela unawasomesha kayumba wakati wangesoma ulaya wangekubeba sana.
Wangeshaolewa na wazungu wana maisha yao mazuri, sio unakaa kaa bar hapa unaona fahari ungekuwa unapanda ndege unaenda kusalimia watoto wako kwa raha, huna akili mzee mwenzangu umewaharibu watoto wako wenyewe naomba usinipangie wala kunishauri maisha yangu!
Basi kuongea vile Baba Pendo akakasirika, akapindua meza akarusha chupa ya pombe kwa Kibopa kidogo impasue uso maana aliikwepa, ngumi kati ya Baba Pendoa na Kibopa ikaanza, watu wakakimbia huku na huko, pombe imeingia mchanga kila mtu akakata mitaa yake nyumbani kwake
Baada ya mwezi mmoja mbele kupita, Pendo akapata simu toka kwa Kibopa, mambo mrembo uko wapi?
Pendo anashangaa leo imekuwaje?
Kibopa: mama mbona kimya? unaendeleaje mimi kibopa, naomba tuonane Sea Cliff kesho ijumaa saa 1 usiku
Pendo: sawa, akakata simu. siku a mjumbe hio hio akatoka mapema ofisini akamfuata mjumbe no 5 kumweleza kuwa Kibopa kapiga simu kaomba waonane kesho Sea Cliff hotel,
Mjumbe no 5: akafurahi, shoga una jota ya jaaaahaaaa! nisubirie nyumbani bado kazi hazijaisha leo nakuletea kungwi akufundeee, usije ukaharibu tena iyo golden chance never comes twice mamaa, hongeraaaa!
Pendo: akaondoka akarudi nyumbani akapika, akafua, akajiandaa kumsubiria kungwi, kungwi kweli akaletwaa saa 2 usiku, Mama wa Tandale ndani ndani huko mswahiiiiliiii ananukia maudi mbayaaaa, kabeba mkoba wake umejaa ma chain ya kuvaa kiunoni, basi karahaaaa, Pendo anashangaa kweli darasa la leo ni kasheshe
Kungwi akafanya yake akatoa aaaalimu duniiiiaaaa kwa mrembo Pendo, Pendo anatoa macho tangu lini ng'ombe akanenepa kwa siku moja, hapa nina masaa yasiopungua 22 kuonana na Kibopa, uuuwi nahisi notes zitayeyukaa mwishoni maana mambo ni meeengi!
Kungwi darasa lilipoisha akapewa chake laki 3 akaacha contact kwa Pendo, shoga ukiwa na swali nipigie muda wowoteee nitakusaidiaaaa, akaondokaaa saa 5 usiku amekodiwa Taxi toka Mikocheni mpaka Tandika huko ndani ndani elfu 50 na laki 3 juuu akafuraaaahii
chezea laki 3 mchezo mchezo, sio kwa kitchen party cha masaa 3 mpenzi msomaji!
Pendo:
Kesho yake muda ulipofika Pendo akaenda eneo aliloitwa, amepeeeeendeeeeeeza mwenyewe katua Sea Cliff na gari ya Mjumbe no 5, wakaongea weeee na Kibopa masaa 3 wanakula wanakunywa, Pendo anashangaa imekuwaje tena na Kibopa kunitafuta baada ya mwezi naaaa!
Kibopa: akaanza kumwaga sumu, Pendo unajua tangu usiku ule tulipoachana sijapata kabisa usingizi, nakuwaza wewe tu kila siku na ile nanihii yako ilivyokuwa safi ya kipekee, inateleza na tamu, sijawahi pata mtu kama wewe hata mke wangu sijawahi kumkuta bikra, sikuamini niliona kama Mungu amenishushia wewe!
Pendo: anashangaa huyu mzee vipi analeta mzaa au ananitafuta kwa round nyingine ya kunichezea?
Kibopa: ndio maana nimejifikiria mwezi na nusu kwa sasa nikaona nikutafute leo, kusema ukweli mimi nakupenda sana Pendo,
Naomba unikubalie ombi la mimi kuwa mpenzi wako wa milele
Pendo: anashangaa heee! hii research imekuwaje tena? mbona kama ishaanza kufeli wakati picha ndio kwaaanza linaanza
Kibopa: Pendo mama, kweli nayokueleza wala sijalewa mvinyo, mimi sijaoa ni mtalaka kwasababu mambo yalikuwa hayaendi
Pendo: akahisi anaotaa? akawa anajisemesha kichwani mwake, Mungu naomba uniamshe maana nahisi naotaaa
Kibopa: akaendeleza sumu kwa mrembo Pendo, Pendo anaona kama miujiza, baadae akamwuliza unasemaje Mama?
Pendo: akaona ngoja kwanza hii research isife, sitaki anione mimi ni rahisi rahisi, akamjibu HAPANA, siwezi kuwa na wewe samahani! akainuka kwenye kiti alichokuwa amekaa akashukuru kwa chakula na mvinyo akaondoka
Kibopa: akaduwaaa! mpare na mawe (hela) yangu nimekataliwaaa? hoooowwww?! akili ikamvurugaaaa!
MWISHO - THE END
0 Comments:
Post a Comment