Bora mchaga mwizi kuliko mpare bahili - sehemu ya 2

 



Chombezo : Bora Mchaga Mwizi Kuliko Mpare Bahili
Sehemu Ya Pili (2)


Manka: hapana mama naona baba keshakuharibu na wewe umeshaanza kufanana nae, hapa lazima baba tumweke sawa haya sio maisha
Si ndio dada zangu au Mnasemaje? !
Mimi bado naendelea kusema sitakaa kuolewa na mchaga kama dada Pendo sijui Nkakeni. Me wachaga staki hata kuwaona na hivi wamenifuata wachaga kibao nimewakaaaajee sasa spendi ujinga na ushenzi na wachaga

Pendo & Nkakeni : ndio je, ngoja kaka aje tuongee nae tuongee na baba kuwa haya maisha hatuyataki tunataka kumfahamu baba yetu
Sio kumwona baba kama kituo cha polisi

Wote wakakubaliana pale wanacheka mama yao anasikitika mara honi ya gari ikapigwa peeeeee peeeeeeee
https://pseudepigraphas.blogspot.com/
Watoto wakapiga yowe baba huyo basi kila mmoja na njia yake kulala, nduki kitandani kulala walishasahu wanataka kuongea na baba yao,
Mama yao akaishia kucheka tu kweli hapa baadae sana akaenda kumkaribisha mume wake mchaga!

Tuonane tar 17 August, saa 8 mchana ya Tz
------------------------------------------------------- 
B. WAPARE ON FLEEK



Sisi wanatuitaga Pare sisters ila sisi tunajiita Dante sisters

Sisi ni wapare wa mwanga, sisi sio wabahili asee kama wale wa Same
Kwanza wapare wa mwanga ni wazuri, wameumbika kama midoli na wana mshepu kama akina Beyonce kifupi sisi ni wazuri afu sisi ni watumiaji wa hela, tupo proud, tunajiskia, tunanata si tuna hela, tofauti na hawa ndugu zetu chokambaya wa same alafu tunajua kujipenda, tunavaaje sasa

Kitandani ndio usiseme, mpare anatoa darasa kwa mhaya na mchaga, mpare akimkamata mumeo wewe utasubiria sana
Nashangaa watu wanasema mwanamke wa singida akimkamata mumeo hawachomoki ila wamesahau wapare ndio no 1
Sasa mdada wa singida anajuaje kuhusu class wakati wamezaliwa porini huko wanavaa manyasi na marangi ya ajabu ajabu kama wanyasa au upinde wa mvua?!
Sisi wapare ni kiboku, tunaitwaga weka mbali na watoto

Lakini ambacho nashindwa kuwaelewa  wa Tanzania wenzangu ni kwanini wanapenda kutuita wabahili

Wapare sio wote wabahili kuna wapare wabahili ila sio wote, labda wapare wa same ila wa mwanga sio asee.. sisi tunatumbua maisha kwa kwenda mbele

Wapare ndio kwetu hapajajengeka kiviiile kama kwa wachaga na wasukuma na wahaya ipo sababu mtaijua tu mbeleni

Naitwa Omana kwetu tumezaliwa wadada 3 mimi wa mwisho, wa kwanza anaitwa Jomana, wa pili Noelina

Tumekulia kijijini Mwanga tumesomea mwanga kuanzia vidudu mpaka darasa la 7 alafu baba akapata biashara Dar ikabidi tuhamie Dar, tukatua Keko magurumbasi tukaanza shule keko form 1 mpaka form 4 baba akapata channel kubwa na networking kubwa ya biashara tukahamia Mikocheni

Hapo ndipo maisha yetu yalibadilika, naongelea maisha ya familia yangu mimi ya kipare wazungu

Shule tukahamishwa tukaanza kusoma za kizungu za academic schools, mzee anaturusha bata batani tunaishi maisha mazuri, shopping kila mwezi tunapelekwa woolworth, tunaenda Kenya enzi hizo Kenya ni hotcake balaa, kusema kweli ukisema wapare wabahili mimi siwezi kuamini maana wazazi wangu hawakuwa wabahili tangu tupo kijijini
Sijui wengine maisha yao yalivyo na wala siwezi kuwasemea

Manka:
Yani wewe Omana kwa kujisifia hauna lolote mjinga wewe
Huyu mwoneni hivi hivi kuna vitu havisemi anajipaisha paisha bure tu hapa

We Omana wewe kwanini dadako Jomana ameshaposwa mara 3 na haolewi yani we mzee wako kazi yake ni Kupokea mahari tu kwani kafanya mabinti zake kitega uchumi cha kupatia hela?!

Mbona dadako Noelina haolewi?!https://pseudepigraphas.blogspot.com/

Omana: we Manka mbona dada zako hawaolewi?! si bora wangu wamechumbiwa !

Manka: sasa yupi afadhali?! Mwenye dada asiechumbiwa na hajaolewa au mwenye dada anaechumbiwa na kuwekewa gundu wanaume 3 alafu haolewi?! Eti Money penny tuambie

Money Penny: nikanyamaza kimya kwa muda kidogo nikamwuliza Manka, kwani kuolewa na kutoolewa kunaingiliana nini na upare?!

Manka: wapare bwana mashauzi kibao hamna kitu sijui vepe me kila siku namwambia Omana acha kujishaua kujipaisha wala maisha yenu hayapo ivyo!

Money Penny huyu Omana, babake sasa hivi hana hata hela, ndio zamani walikuwa na hela, wakasomeshwa vizuri sana mpaka chuo na kazi dada zao wanafanya ma benki wana nafasi nzuri ndio wanafunika wazee wao na hata hapo mikocheni wameshahama wanaishi kunduchi kiwanja ambacho babake alipewa zawadi na rafkiake ndio akajenga hapo kwa mkopo wa bank dada zake Omana wamechukua kazini nyumba ikaisha vyumba 3 ndio wakahama mikocheni vinginevyo wangerudi same sijui mwanga sijui Moshi hana lolote

Money penny: sasa wewe Manka mbona unaonekana kama una hasira na wapare au na Omana? ! Mnanichanganya

Omana: eh mwambie dada penny, ahahahaha uuuwi kweli wachaga na wapare hawawezi kaa chungu moja ndio maana mababu wakatufanya watani wakamaliza ugomvi

Manka: Yani da penny Ngoja nikupe ukweli wa Omana,  huyu bibie anapenda maisha flan ambayo kwao yalishaisha, huyu omana huyu mwone hivi hivi ni kahuni balaa!
Tena huyu usijejiloga penny ukamwonyesha mumeo utajuta! Yani mmmh we acha tu

We Omana wewe si unaendaga na kwa waganga wewe au sio wewe?!
Juzi kati kaenda bagamoyo hapo sijui kuna mume wa mtu gan amempata ana hela, ka Omana kanapenda mabonge ya bwana hataki kukubaliana na hali ya familia yake anataka mambo makubwa tu na hata baba yake alishamweleza ila ni kichwa panzi hatari

Kamwendea baba wa watu kwa mganga bagamoyo, uzuri mke wa huyo baba ni mlokole Omana akashindwa
Alipoona ameshindwa akakaa kimya

Baadae akaja kupata bwana mwengine mfanya biashara mkinga ana maduka kkoo eti kamwendea kwa mganga kwao same sijui mwanga weweeee huo ugomvi wake sasa skuhio tupo pale ifm tu na discuss usiku akaja mkinga wake kwa jazba anamwita akajua kimenuka
Akaniambia Manka nisindikize nikija kuuawa wewe shahidi
Kwenda kuskiliza ugomvi bwana mkinga nae mchawi vile vile akamwambia Omana we mwanamke unataka kuniloga mimi utakufa kabla, mimi nimekupenda kama ulivyo na wala sijatumia dawa nina mke na watoto nyumbani lakini nimekupenda sijakuzuilia kupata vijana wenzako kabisaa wala sijakuendea kwa waganga
Sasa kama unataka kuniloga utakuwa chizi wewe mtoto utajuta kuzaliwa akaondoka mkinga wa watu me namshangaa Omana anajiliza mshenzi mkubwa

Ndio siri ikatoka Omana anapenda kwenda kwa waganga tangu skuhio Omana hana mashauzi na mimi kama anaendesha maisha yake na masomo kwa nguvu za giza asithubutu akaniloga mimi half-cast wa kichaga.. wagogo kwa mama wana dawa kuliko wapare na wamachame ndio usiseme

Ndo ivyo penny hawa wapare hamna kitu ubahili tuhttps://pseudepigraphas.blogspot.com/

Kwanza penny huyu omana ni mbahiiiiliiii hakuna mfano na ana roho mbaya sana nadhani dada zake wapo ivyo ndio maana wakichumbiwa wanaume wanakimbia kabisaa
Roho mbaya na uchoyo kwa wapare unawafanya waitwe wabahili
Juzi kati nilipoteza hela bwana nikamwomba kwenye simu Omana nisaidie basi elfu 30 nimalizie pepa nikienda home nakuletea kanikatalia katu katu
Basi nikaomba mshikaji m1 akanifadhili na elfu 20
Baada ya dk 30 akaja Omana chumbani akaweka wallet oh me naenda chooni nishkie
Kumshikia wallet kufungua nakuta ana laki 3, nikachukua elfu 30 nikajikausha
Akaja mwenyewe katoka chooni, anajiongelesha oh me sina hela me namwangalia tu Omana ananiadithia sijui karudiana na mkinga mambo mazuri ameshasahau nimemwomba hela anikope
Baada ya dk 20 akaondoka hajui kama nimemwibia elfu 30, we Omana mchoyo sana una roho mbaya mtoto wa kipare na ukiendelea hivi utakufa vbaya

Omana: ahaa kumbe ndio wewe uliniibia elfu 30 yangu ee kweli wachaga wezi, bora umejisema nipe hela yangu haraka

Manka: wala skupi kwanza sina

Omana: nipe bwana tutagombana!

Manka: mmmh wapare bwana, njaa tu

Omana: kama wewe ulivyo na njaa mpaka ukaniibia  mwizi mkubwa wewe nipe elfu 30 yangu

Manka: akatoa elfu 30 akampa na akatoa na elfu 10 akamrushia usoni, hio utakunywa soda maana umetoa povu sana kila mtu hapa hotelini anakushangaa

Money Penny nikacheeeka nikacheka mpaka Omana akaamua kuondoka kwa aibu na ile elfu 10 kaichukua, cheza wapare wewe ??????????????????
Shikamoo Wapare!




Tuonane Tar 18 August saaa 12 jioni ya Tz
---------------------------------------------------
SEHEMU C. TEA PARTY

PALM BEACH Hotel

Kila baada ya miezi 3 warembo 5 hukutana kwa ajili ya tea party si unajua tena mambo ya kikundi hivi bikini vyetu vya kibongo bongo ??

Moja kati ya warembo hao alikuwa Omana, Manka, Doreen na Elizabeth

Omana na Manka kama unavyojua ni wapare na wachaga, Doreen ni Mpare na Elizabeth ni Msukumahttps://pseudepigraphas.blogspot.com/

Basi wanakutanaga kwenye Tea Party wanadiscuss mambo yao ya kikundi na maendeleo, wanaongea mambo mengi ya masomo na maisha Baada ya masomo na mambo ya mapenzi blah blah blah!


ITAENDELEA

About THE STORY BOOK

0 Comments:

Post a Comment