Bora mchaga mwizi kuliko mpare bahili - sehemu ya 1

 



Chombezo : Bora Mchaga Mwizi Kuliko Mpare Bahili
Sehemu Ya Kwanza (1)


SEHEMU YA 1

A. MAMA MIMI SIOLEWI NA WACHAGAAAA

MANKA:
Yani mama mimi sipendi kabisa kuolewa na hawa ma shemeji zako wa kichaga  me hata sielewi kwanini uliolewa nao mama ilikuwaje ukaolewa na wachaga!

Mama Manka: ah acha tu mwanangu huyu babako lakini nampenda
https://pseudepigraphas.blogspot.com/
Manka: hapana mama haya sio maisha tunayoishi asee. Mzee ana hela ana mawe lakini tu naishi kama watu mafukara jaman

Angalia familia ya akina Eliza na akina Ngosha pale angalia akina Lulu wanavyoishi jaman huyu baba sijui yupoje kwanza amerudi baba maana akiniskia nitajuta kuzaliwa

NKAKENI: kwanza mama hii Tabia ya baba kila akirudi nyumbani watoto tunamwogopa kama Mungu ni nini?!

Kwanini tusiwe kama akina Ngosha pale baba yao akija tu wanamkimbilia wanamkumbatia wanaenda nae ndani
Sisi baba akija kila mtu kulala na hapo uwe umefanya homework, haya maisha siyapendi kabisa

Manka: alafu Tabia ya kutulazimisha kwenda Moshi Moshi kila mwezi wa 12 kama wafungwa nimeshachoka me staki.. sasa hivi nimeshamaliza sekondari naenda chuo nataka uhuru wangu. Nimefaulu form 6 sawa naenda hapo Ifm kusoma yani nataka nikae hostel niishi maisha ambayo Mungu amenipangia kuishi sio haya ya Mungu shetani Binadamu
Mungu akitokea shetani anakimbia
Shetani akitokea Binadamu anakimbia nimeshachoka asee
Nataka nikienda chuo niweze kujirusha,  niwe na kula kuku mzima sio hapa nyumbani ni vipapatio tu Tangu wadogo mpaka wakubwa ni nini
Me mpaka sahivi sina bwana, sijui hata kupenda, sijui chochote kuhusu wanaume wanaume nawaona kama Mungu maisha gan sasa haya!?

Nkakeni: kuhusu kula kuku, kwanza mpaka twende sabasaba au twende Moshi Krismas ndio tunakula

Haya hapa nimepata mchumba anataka kunioa najiuliza naolewaje wakati baba namwona kama chiu

Mama; oh mwanangu umepata mchumba hongera sana sasa analeta lini mahari? !

Nkakeni: mahari?! Mahari nani analeta nimempiga stop staki mahari maana ni aibu na huyu baba yetu ushuzi mtupu sio kwa mateso haya ya hapa nyumbani manina kabisa huyu mzee me mama nitakuja mfanya kitu mbaya mpaka arudishe namba

Mama: kwaiyo unataka kumwua baba yako?!

Nkakeni: simuui ila nitafanya kituko hatari mpaka apate presha ya kushuka na kupanda ataondoka mwenyewe atuachie sisi tushikilie vizuri watu tunaishi kama tupo mafia au Sudan kusini kwenye vita kumbe tunaishi kwa wazazi

Pendo: ivi mama huyu mumeo anajua kupenda kweli? Kwanza ulimpatia wapi maana wewe sio wa kabila hili wewe ni mtu wa Dodoma

Mama: mh jaman mbona mmeniandama?! We Nkakeni unataka kuolewa wakati shule ndio kwanza form 4 umemaliza acha ujinga usome mpaka chuo upate kazi. Baba yako hatopokea mahari bora umrudishe huyo bwashee wako

Manka: eh dada Pendo, unakumbuka tuliendaga Moshi juzi kati kwa ajili ya christmass bwana si shangazi akawa anaongea na marafkizake anawaambia wifi yake ni Chyasaka?!

Pendo & Nkakeni: eh niliskia nilitamani kumpiga shangazi na jiwe kama sio kaka kunistopisha alinikera sana shangazi
Hawa wachaga me siwapendi hata tone
Angalia baba ana hotel 3 daslam. .. Ana hotel 1 Moshi. .. Ana nyumba 3 dar za kupanga, anafanya kazi serikalini ni boss lakini watoto wooote tumesoma shule za kayumba kuanzia vidudu mpaka chuo labda kama Nkakeni atapata bahati ya kusomeshwa shule za uzunguni
https://pseudepigraphas.blogspot.com/
Mimi kama dada yenu Pendo staki kabisa kusikia habari za kuolewa kama wanaume wapo kama baba yangu basi wakae na mavuzi yao staki kabisa kuwaona

Mama: akainama chini analia maskini mama wa watu, wakawa wanambembeleza pale ikabidi maza afunguke kabla mzazi hajarudi

Unajua nimeumia sana pale Pendo Aliposema hataki kuolewa tena imeniuma sana. Pendo naomba ufute hio kauli haraka sana maana itakutesa kweli

Miaka ya 70 nilipomaliza shule form 6, wazazi wangu wote walifariki katika ajali ya bus, wakitokea dodoma,

Wazazi wangu walikuwa wanapendana sana sana
Tangu hapo nikaja kulelewa na jamaa ya baba alikuwa mchaga, alinitesa sana hakunijali... kuamka asbh saa 12 kukatia ng'ombe majani na kurudi kukamua maziwa mpaka uje kunywa chai ni saa 4 asbh, chakula cha mchana saa 9 jioni cha usiku saa 5 usiku Kuamka asbh saa 10 asbh
Maisha yakawa magumu elimu yangu ya form 6 ikaishia hapo hapo sikuweza kwenda national service wala wapi nikawa mkatia ng'ombe majani wa jamaa alienichukua
Kwetu nimezaliwa msichana peke yangu,  sikuwa na ndugu na wazazi walipokufa nikabaki mwenyewe

Basi nikakaa na wale watu miaka 5 siku moja akaja baba yetu toka kijiji kingine cha huku moshi, akaniona akanipenda akawa ananitaka me namkataa kwasababu sikuwahi kuwapenda wachaga kabisaa kwa yale mateso ya yule baba na mkewe

Hapo natamani kutoroka sipati chance nakamatwa kila nikipanga,
Nikajua na kichaga, na yule baba alienichukua alikuwa anawaambia mimi ni mtoto wake so wale majirani pale wakawa wanajua mimi mchaga nikitoroka nadakwa na majirani pale narudishwa nachapwa nanyimwa msosi siku 2, naliaaa weee baadae nanyamaza

Siku 1, ilikuwa usiku wa mwaka mpya pale kijijini kwetu Kilimanjaro, wakawa wanachoma matairi shangwe za hapa na pale, wanapika pombe za makunduuu  (makunduu ni ndizi za kupikia pombe ??)



Nikawa nimekaa kwenye kijiwe naangalia watu wanasherehekea mwaka mpya wa 1978
Sipo mbali na mlango wa nyumbani buzy nakunywa pombe ya makunduuu
Mara naskia mtu ananikaba mdomo na shingo akanipiga kichwani
Kuja kuzinduka niko kwenye chumba cha kitanda kimoja, mh nikajua naota nikarudi kulala
Baadae kuja kushtuka kweli sipo nyumbani kwa yule jamaa nikaanza kupiga kelele akaja kijana mmoja ananifokea unanini wewe mwanamke shida nini?!
Hujui kuwa umeshaolewa?!

Nikajiuliza nimeolewa?! Namwuliza kivipi sasa?!

Kijana: nimekuoa jana usiku nimekuoba kwenye mkesha na leo yameshapita masaa 18 yakifika 48 hawakuoni nyumbani basi wanajua ushaolewa
kuskia hivyo nikapiga makelele majirani waje lakini hamna majirani wala nini kumbe kanificha porini huko hamna watu mpaka utembee km 5 makusudi akijua kule watanitafuta

Basi kweli baada ya masaa 48 kweli bwana me nikawa mke wa kuibwa nikarudishwa kijijini kwao machame
Nikakaa mke wa mtu basi hali nikaikubali sasa nifanyaje labda maana nimeruka majivu kwa kukanyaga motooo
https://pseudepigraphas.blogspot.com/
Miezi 9 ikapita nikamzaa kaka yenu huyo huko kijijini, baadae maisha yakawa magumu mume wangu ambae ni baba yenu akaumwa sana karibu ya kufa, wazee wa baba yenu wakakaa kuumizana kichwa wakajua aliniiba mkesha wa mwaka mpya, Wakamwambia mrudishe mtoto wa watu ukamuoe vizuri upya umekosea sana mizimu inaita
Basi nikarudishwa kwa yule baba jamaa na kakaenu, akafurahi kutuona na mkewe wazee wakaongeaaa wakaomba msamaha pale yule jamaa alienilea akakubali akasamehe wakalipa fine ng'ombe 30 na mbuzi 20 na kondoo 5, zikaletwa ndani ya siku 3, wakaomba dua pale basi mume wangu akapona pale pale akawa mzima

Wakatufungisha ndoa kesho yake na mchungaji alikuja nikaolewa sasa na baba yenu huku nimeshazaa mtoto wa kwanza kaka yenu

Baada ya siku 5 za mila na ndoa tukarudi kijijini kwetu machame kwa mume pamoja na wazee na kakaenu.. kufika baada ya siku 2 babaenu akapigiwa simu amehamishiwa kikazi dar es salaam ndio tukaingia dar es salaam mwaka wa 79, kaka yenu akiwa na mwaka mmoja tukaingia daslam kwa baraka za wazazi wote

Tukawa tunaishi Kijitonyama mpaka akazaliwa Pendo akaja Manka akaja na Nkakeni ndio tukahamia Upanga tukaishi hapo wee mpaka mwaka wa 2000  tukahamia mbezi beach enzi hizo mbezi beach ilikuwa hot cake sana, lakini ilikuwa inasikika kama mbezi beach ya majambazi

Ndio mpaka leo tupo hapa mmezaliwa hapa mmekulia hapa mmesoma hapa wengine kuanzia nursery mpaka chuo mpo hapa nyumba ya mbezi beach

Ila ndio hivo kuwachukia kwangu wachaga hakujasaidia maana ukatili niliofanyiwa na baba yenu ndio niliofanyiwa na baba mlezi wangu

Sikutamani kuolewa kabisa lakini nikaishiwa kuolewa na wachaga hao hao niliowachukia
Sasa nyie watoto mnataka kuleta revolution ipi tena wakati maisha yenyewe ndio haya haya, Kubalianeni na hali zenu acheni tamaa
Kubalini kama mimi tu angalau mimi mke baba akiacha paja la kuku nakula
Na nyie subiri mkiolewa mtakula vinono pia

Pendo team mate chini kabisa maneno yasijekukurudia Yeleuuuwi team mate kabisa chini kiruwai... wai!https://pseudepigraphas.blogspot.com/

Sasa kwanini watoto wangu hamtaki kuridhika na maisha haya tulionayo?! Mbona ni mazuri sana kuliko yale niliokuwa naishi mimi.

Manka: haya sio maisha mama wewe ulivyokuwa na huyo mlezi wako ulikuwa unamwangalia kama Mungu flan na kumwogopa!? Chakula hamli pamoja, mawekwa jikoni, kumwona baba mpaka sikukuu hii ni sheedah mama

Mama: ndio tena me nilikuwa nakula jikoni na mbwa na ng'ombe si bora nyie mnakula chumbani kwenu mshukuru Mungu basi na hivi mimi ni mama wa nyumbani hata sijui mtafanyaje. Lkn angalau mmesoma mpaka chuo na kaka yenu anayo ajira angalau mtanisaidiaga huko baadae


ITAENDELEA

About THE STORY BOOK

0 Comments:

Post a Comment