ON MY HIGH HORSES PART 2


Chombezo : On My High Horses
Sehemu Ya Pili (2)


They call me a woman without a soul, poa tu, siwalaumu. I vacationed in hell tangu babangu afariki, lakini sasa Mbingu inani considers mimi mtoto wake haijalishi nalewaje but Heaven knows my name
Sijali wanayosema kuhusu mimi, this is me, Gigi le gigi.
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Tangu niondoke kwenye ile nyumba ya mama mkwe maisha yangu yakabadilika sana, nimetoka kuwa from being a toxic girl to a wiser lady, i didnt murder my husband kama wanavyosema, poor guy dropped dead right b4 my eyes

If it wasnt for this mahakama and crap to put me one AA meetings ningeshaondoka Tz siku nyingi na hivi mama yangu alifariki mwaka juzi sikutaka kabisa kukaa hapa Tz, ningekuwa America nakula zangu bata maana hata sioni nafanya nini tz, sina wazazi walishakufa, kwetu nimezaliwa mwenyewe, ndoa imekufa am all alone, i cant wait kumaliza hizi AA Meetings wanipe visa niondoke, kha!

Kwa leo naomba niishie hapa alhamisi nita share tena ila kwa kweli nina amani kuwa nimeshajua kwanini baba yangu alifariki na nani amemuua!

Inatosha acha niwe sober nikaanze maisha nchi nyingine kukaa Tz mama mkwe atahakikisha na suffrr mpaka nakufa!

That mama mkwe ni mchawi na muuaji, mmeskia nyie clowns kwenye camera mnaoniskiliza, sijali how much amewahonga now i have an inner peace, nimeshajua nani amemuua baba yangu, nimeshasamehe hata kama mama mkwe ni tajiri amekaa kwenye high horse yake haijalishi the victory is all mine now and soon nitamfunga tu mama mkwe, na soon atakubali kuwa amemuua baba yangu!

Wagonjwa wote wakaangalia kama Gigi ni mkichaa kidogo au?wakashindwa kumwelewa

Doctor Grace:
akachoka na maneno ya Gigi akaona kwa leo tuishie hapa tuonane alhamisi saa 1 usiku, wakatawanyika lakini Aaliyah akampenda sana Gigi akamfuata akamwambia Gigi me naaamini kuwa wewe ni mtu mzuri sana, hata kama tunaitwa walevi lakini sisi sio watu wabaya, naomba niwe rafkiako

Gigi:
utaniweza mama?! Me mambo safi ivooo

Aaliyah:
utanifundisha vitu vingi sana kwenye maisha hata kama ni maskini najua hatutashindwana,
Mbona mzee guibu mmewezana, naomba niwe rafkiako

Gigi:
akamwangaliiiaaaa, akamwambia poa ila inabidi uwe kamanda uache kulia lia, me siongozani na wanawake chickens mnalia lia uchuro tu hapa unakomaa ukiwa na mimi, ukilia nakupigaaa staki ungese

Aaliyah:
poa boss no problems
Wakabadilishana contacts wakaondoka pamoja kuelekea kwenye gari




TUONANE TAR 27 FEB 2018 SAA 1 USIKU YA TANZANIA
________________________________

C. TAUSI THE SWEETEST


TAUSI

"Kusema ukweli mpenzi wa Mungu na Mungu yupo amekaa juu ananiona, yani yani yani sikujua kabisa kama Aaliyah amekuwa snitched na bonge jaman.



Wanaume ni madudu washa washa hakuna mfano wake yani ni madudu washa ambayo mpenzi msomaji kama una hamu zako wewe watumie tu ukiwa na uondoke wala usiwaweke moyoni maana utakufa na kupasuka moyo



Best Friend wa Mark kuja kunieleza tena ananisuta kwakweli sikumwelewa wala kumwamini.



Inakuwaje me nimjue mark anaoa best friend wangu bongee alafu nisimwambie swaiba yangu Aaliyah. Ndio bonge ni rafkiangu tena best ila ningekuwa najua uhusiano wa Mark na Aaliyah nisingempeleka Aaliyah kwenye harusi.



Ujue pesa kitu mbaya sana, mimi ofisini ni secretary, nipo Tazara pale, na kazi amenitaftia mamake bonge, akanipa mil 3 kama zawadi nilipopata kazi, sasa mpenz msomaji, 1 week kabla ya harusi ya bonge mamake bonge alinifuataa akaniambia kuna kazi



Nataka unifanyie favor moja akaweka mil 10 mezani.


Ati mil 10 nakwambiaaa.

Mshahara wangu laki 150 tu.

Embu nambie laki na nusu naletewa hela mara 100 ya mshahara wangu naambiwa kuna mtu nataka ufanye nae urafiki tuu.

Umteke akili awe rafkiako tuu, umwaminisheee awe best yako. Nikapewa Miaka 3 tu na picha na shule anayosoma na nyumba anayoishi na familia yake. http://pseudepigraphas.blogspot.com/

Basi nikaanza u ditective wa kujitolea wa kulipwa mpenz msomaaji. ndani ya miaka 3 namfuatilia mrembo Aaliyah.

Mpaka anamaliza mwaka wa 3 anaanza kazi nishajua mingle zote, mama bonge akaniambia muda wa kuzoom umeisha sasa nataka uanze urafiki nae.

Nikakutana nae ana drive nikamgonga makusudi ilikuwa siku ya mvua. Nikaomba msamaha Aaliyah akakomaa.

Tuka exchange contacts nikamtengenezea gari yake Rav 4 zile old version 3doors. Mpaka namaliza matengenezo ni mama tu anagharamia.. Matengenezo wakati yanafanyika nikawa rafiki wa Aaliyah mzuri tu


Mpaka gari inapona dadeki tukawa tusha hang sana tu mara kutafuta spea mara kulipana mara nini ah si unajua tena matengenezo ya gari me namwambia me mweupee sijui spea sijui vifaa tangu niendeshe gari sijawahi kugonga yani secretary ditective flan amaizing ivi.


Gari imepona tukawa marafiki, mimi namdanganya nipo single yeye kwenye rlshp.

Lkn sikuuliza sana kuhusu mahusiano yake maana sikutumwa ivyo.


Mwaka jana mama bonge akanihamisha uswahilini kinondoni kwenda mbezi beach njia ya chini, nyumba ya chumba kimoja akalipa rent miaka 2, kweli mama bonge bwana alikuwa amejidhatiti vbaya mno..

Na sikujua kwanini alikuwa anamfuatilia sana Aaliyah.. Kumbe ni Mungu kuhamia mbez beach aaliyah akataka kupafaham kwangu akaja na bwanake Mark, ndio hapo namfaham mark.


Wakakaa kama 2hrs wakala wakanywa wakaondoka.
Baada ya wiki 1 nimekaa zangu hm weekend akaja MARK na migenye yake.. Oh mimi nipo vibaya na Aaliyah, anipi shoo
Naomba nistiri nina miezi 6 sijapata shoo.

Ah nikamkazia kimtindo akaning'ang'ania sana, nikaona what the hell?

Mimi mwenyewe natembea na mume wa mtu je na ivi kaenda uraya acha nijisevie, nikajisevia sevu sevu na wewe, mechi ikachezwa na mpira je, kha! Mark ni noumer.

Mark bwana sina wa kumfananisha mpaka sasa, maana nimecheza na mabazaz wote hata mume wa mama bonge alishanitokea nikamgawia moja tu basi ndio kuchonga mzinga mpaka kukamatwa na mama bonge, ilikuwa patashika roho kuinama, yani niacheni tu mie ndo tausi kama hauna moyo kama wangu unaweza jiua

Mama bonge akaniweka chini akaniambia wewe ni mwanangu mume wangu namjua fikaaa, pole tusahau yaliopitaa, bonge kaniambia hauna ajira ntakutaftia mwanangu, hakuonyesha kukasirika akawa anamlaumu mumewe tu..

Skuamini mpenz msomaji, nikajua mama amesamehe kumbe kaniweka chamboo ndio saivi nimefanyika punda wake, nalipia dhambi ya kufumaniwa mpenz msomajii.

Mimi sina kosa kwa yale yaliomkuta aaliyah lkn najua mama ananiadhibu akina mama wengine Mungu awasamehe tu nadhani moto wa milele ni wake

Turudi kwa Mark;

Unajua Mark alinichukulia poa sana akadhania me cheap thriller kumbe me bad ass, kazi nazofanya ni za kijesusi tosha CIA wanakuja kuchukua twishen kwangu, me mtoto wa singida, singida og.

Mtoto mweupe, sina chura mimi slim body, lkn nikimkamata mumeo habandukii..

Mume wa Mama Bonge aliponitega kitendawili mpaka hii leo ameshindwa kuniteguaa..

Nipo na mume wa mama bonge mwaka wa 4, tangu mama bonge amenifumania tukaendeleza ibada ya milele, mzee kanogewa basi ndo kugewa pesa, nishanunuliwa nyumba mikocheni A, jina langu imagine me secretary wa Tazara ninamiliki nyumba kwa washua.


Sasa Mark bwana akaja na kipepsi chake me namzoom tu anavyotaka kunipagawisha kumbe me sipagawishwi.

Akanifunga kibao ki 1 akajiona kiduume tukalala mimi najiona kama amenitekenya
Round ya 2 akaamka na hamu zake tena nilimshiiikaa, nikamweka chini me juu mambo ya horse riding, wee mwanaume analia oh tausi tausi mama tausi nisamehe nilikuchukulia poa , bebi utaniua wee, uuwi yeesu na maria, tausi nibo buzy na nyanyo tuu, mark analiiiaa, yani very stupid man, nikarudi kulala akawa anahema juu juu, kukakucha amenogewa anataka tena, ah nikaona anataka kunichosha tu mjinga huyu hana lolote nikajifanya napokea simu eh bebi unakuja?
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Saa ngapi?

Baada ya nusu saa?

Karibu sana mpenz, nikajifanya simu imekatwaa, eh we Mark amsha amsha, mume yupo mtaa wa pili haya haya fasta ondoka plz plz plz sepaa, akachukua nguo anavaa fasta fasta kama amefumaniwaaa,

mimi namcheka rohoni stupid boy, anava boxa fasta fasta anachekeshaje sasa, mara anaanguka mara anakosea kuvaa shati mara kageuza suruali aki nikabakia nacheka viatu na soksi kaenda kuvalia kwenye

Gari chezeiya fumanizi wewe?

Akaondoka na gari yake hamna cha mtu yeyote aliekuja nikarudi kulala..

Mchana akanipigia sikupokea, usiku ckupokea, kesho kutwa asbh akapiga nikamdanganya nipo kanisani nikaweka nyimbo za kwaya kwa nguvu akajua kweli, mchana akapiga nikamtext nipo kwa dokta wa Meno siwezi ongea,

usiku akapiga nikamtext mdomo umevimba we tuma sms nimefanyiwa root canal, nimeambiwa kuongea baada ya wiki akajibu poa


Wiki ikapita akapiga nikakata, akapiga nikampa mfagiaji ofsini anamwambia we nani

Mark: mimi bwana wake

Mfagiaji: basi mkeo kapata ajali hapa me nimefanya kuiba simu uje maeneo ya mbagala kizuiani utamkuta, ukikuta wameshaondoka uende polisi braza me hii simu nimeiokota mbali ila naichukuaa

Mark: hapana bro usifanye ivo me ntakupa hata mil 3 tuonane mbagala unipatie plz,

Simu ikakatwaa, nikampa buku 3 mfagiaji simu nikazima

Nikaweka namba yangu ya ujesusi ambayo hata Aaliyah hakuwa nayo ila
Baada ya miezi 6 nkarudisha namba yangu ya zamani.

Hakunitafuta tena mpaka bonge ananiambia anaolewa, na kuja kumcheki kwenye sherehe namwona Mark ndo bwana harusi ngachokaa..

NIkamhurumia sana bongee maskini yule Mark atamcheat maana anaonekana njaa balaaa, tena njaa kalii, atampiga mama bonge lkn hata kumcheat bonge kuko moja kwa zotee sijui kwanini Aaliyah alichanganyikiwa angeendaga tu kanisani akamshukuru Mungu maana sio kwa msalaba ule alioutuaa, akamshukuru Mungu tu bila ubishi


Kitu ambacho haujajua mpenz msomaji ni kwamba kabla ya Honey Moon Mark alikuja kulala kwangu kwa malalamiko kwamba bonge bwana hajampa uroda tangu ashike mimba..

Nikamwambia mimi free dushe sipokei akazama mfukoni akatoa mil 1.

Akaweka mezani, nikamsevia ya kishkaji kama ya sku za mwisho, Mark alikuwa wamoto sana sana sana, meaning hajambato muda yule na hivi kwa Aaliyah alishaharibu am sure hajalala na mwanamke muda sana..

Cha ajabu zaidi walipoenda honey moon siku ya 2 Mark akaja kuweka hema kwangu hapa masaa 2, nimepigwa mbupu hapa kama me bi harusi, pesa za kamati ya harusi ya Mark nimekula sana, kaja kwangu siku ya 2, 3, 4 na ya 5 ya honey moon anataga mil 1 kila siku kwa masaa 2, ndani ya siku 5 kabla na baada ya honey moon nina mil 5 kuhudumia bwana harusi.

Mark hana akili kabisa, mark hana rohO ni skeleton jinamizi la kuzimu na jinsi walivyokuwa wanaangaliana na mama mkwe wake kwenye harusi, lazima Mark amemlala mama mkwe..

Me nakwambia sio bure haiwezekani mark amwache Aaliyah kwa ajili ya bonge michellin, ngumu kumeza yule Mark kafuata pesa za mama bonge tu si tupoo, utanambiaa

Sina shida na jinsi Mark atakavyomla hela mama mkwe wake na wala hainiumi si kila mbuzi anakula kwa urefu wakamba yake bwana haisumbuiii lakini pale ndoa ikimaliza mwaka utaniambia mpenz msomaji mIMI naomba niwe shahidi wa familia ile!"





Tuonane alhamisi Tar 1 March 2018 saa 1 usiku ya Tanzania

_______________________________

D. Mama Bonge (mama michellin)

"Iron Lady on her High Horse"




"Watu bwana, MIMI hata siwaelewi, nimeshawasaidia sanaa, tena sana tu lakini sikuzote shukrani ya punda ni matekee, acha wanipige mateke wanavyotaka na mimi narudisha

Wengine wananiita iron lady wengine wananiita roho mbaya wengine wananiita kuni ya moto wa milele wengine wananiita jezebel, hata sijali mimi nasema SIJALI


Mimi hapa nina miaka 55, nina watoto 3 wakike 2 kiume m1, my son nampenda saanaa sana sana sana, lakini ndio wanadamu bwana wanadamu sio watu wameniulia mtoto wangu wa kiume, my only son nampenda sana kama baba yangu wa kunizaa mwenyewe lakini basi nishasamehe tenaaaa. Nasubiri wajukuu labda Mungu atanipa wa kiume toka kwa bonge wangu

Dadake bonge mwanangu wa pili amezaa watoto mapacha wakike tuu baada ya hapo fibroid ikamchukuaa kizazi , ilimla sana kizazi wakamchomoaa huko Uingereza.

Ila watoto ni watoto tu, wajukuu vile vile ila ndio kaolewa mbalije sasa? Kaondoka nyumbani sina ukoo tena, uzuri mwanangu bwana kaolewa pazurijee, hapo hatokufa maskini naweza kulala mauti bila kufurukutaaa kaburini

Bonge wangu shukrani Mungu ameolewaa maana zile KFC buana zimemchanaa balaa kuja kumkuta hamna kiuno wala shingo wala nini, akyanani, nimempeleka gym wapi, nimempa ma diet suppliments za kila network marketing zimedundaa basi nikaona tu sasa nimtaftie mume
Kumtaftia mume bonge wangu ilibidi ni invest sana kumtaftia mume.

Katika spot spot zangu na kutafuta wakaka wa maana watu wazima bahati ikamdondokea Mark.

Mark nilikutana nae Kempinsk hotel ya dar, kumwona nikampenda sana na alivyo mkarimu, mchangamfu, kwa watu wote, nilimkuta reception pale alikuwa anamchangamkia receptionist nikasema hapa hapa team sibanduki

Nikamfuatilia kujua yupo na kadem kake kametoka nako mbali wai nikaamua kuingia mzigoni, nimeinvest sana kwa mtoto bongee, bonge ingawa kanajielewa she's worth investing for...

Nikamnunua Tausi pale kwa miaka 3 tangu nimemspot Mark kwa Tausi nimetumia mil 20.
Ndio mil 20 za kibongo, tena na zaidi lkn acha tufanye 20 kwa sasa, ila mkataba wangu na Tausi umeisha pale ambapo bonge aliolewa.

Hela zangu kwake zimekata, ila sasa ataisoma namba, si alitembea na mume wangu mara nyingi hata nilipomkamata bado aliendelea, ataisoma namba sana tuu sio kwa maisha haya

Yalioshuka tuone sasa ataishi na nani mtaani na madharau yake na hivi anamtegemea mume wangu ataisoma namba..

Kuna kitu lazima nikueleze uelewe kuhusu mume wangu nyie hamjui tu
Mimi kwetu kwa wazazi wangu tulikuwa matajiri sana tukazaliwa wa2 tu mimi na kakangu. Wazazi walikuwa wana heraaa mpaka serikali ikamchagua babangu kuwa chief akawa anaisaidia serikali ya kijiji, wazee kabla hawajatangulia mbele za haki wakatukalisha chini maana walikuwa wasomi wa UK, hasa baba yangu..

 Nadhani unanielewa mpenz msomaji nikisema kuwa babangu ni wale ma graduu wa kwanza enzi za Mwalimu waliosoma UK, sio mchezo ni ngumuu.. Sukari yenyewe enzi za mwl sheedah, to cut the story short mzee akatuita mimi na bro wakati tume graduate, akasema jamaa me siku zangu za kuishi zimebakia chache ila kabla sijaondoka kuna mambo nataka kuyaweka sawa kwenu.

Naacha uridhi, kwenu wote nusu kwa nusu under 1 condition, kabla hamjaoa
Au kuolewa naomba msainishe wake na waume zenu Prenap. Najua kwenu mnaelewa prenaptual aggreement ni nini, sasa mkaolewa na kuoa wasio wasomi mnakazi ya kuwaelewesha.
Wakisain prenap ndio mnaweza kupata mali zenu za uridhi vinginevyo urithi sahauni..

Ikatokea hammjaoa au kuolewa kuna aina nyingine ya maelezo kuhusu urithi. Me naamini mtaoa na kuolewaa.
Sasa huu uridhi bwana utawalenga mpaka vizazi vyenu vya 4. Mume au mke akisumbua akaondoka mali zinabakia kwenye familia kwa vizazi na vizazi

Mali za wajukuu zinaanza kutolewa pale wakioa au kuolewa tu na sio vinginevyo na pia kabla hawajaolewa au kuoa lazima waume au wake zao wasaini prenap

Ikatokea hamjaoa au kuolewa mkazaa tu pia prenap ya wajukuu itolewe watakapooa au kuolewa na lazima wasainishwe prenap hao waume zao. Hali hii iendelee mpaka kizazi cha 4. Muwafundishe wajukuu na vitukuu jinsi ya kusimamia mali.. Sawa?

Mimi na kaka tukasema sawa mzee
Basi bro akaoa uzuri mke wake msomi mwelewaaa...akakubali ku saini kila kitu ndoa ikafungwa mpaka leo wapo pamoja yule wifi katuliaa chezeiya mali wewe mjini dar wana nyumba 5 wana tower kkoo, mikocheni, bado hisa, bado mashamba, nyumba Dubai, SA kiru kakangu nomaa

Mimi sasa mimi utanihurumiajee
Kila bwana naempata anajiona duni, mmoja akaniambia kuwa hawezi nioa akinioa ni sawa na kuoa mwanaume mwenzakee

Nikamwacha aende zakee
Nikasota wee wote niliosoma nao walishaolewaje sasa, walisha zaaje tenaa wameshamaliya me zeroo.
Nikaona uridhi wangu kuzaa, ktk pita pita zangu kibiashara nakutana na mume wa mama Gigi ambae ni marehemu sasa.

Tukapendana wee nikajua naolewaa, bdae anakuja kunambia amempa mimba ex wake ambae ni mama gigi na walishaachana, ila alimwachia ujauzitoo ana mimba ya miezi 6 na wazazi wa mama gigi wamekuja juu wanataka aoe kwanini wamemwaribia mtoto wao usichana wake, ndio baba gigi
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Kaniachaa akamwoa mama gigi ana mimba ya miezi 7... Niliumia sanaaa ka gigi kakazaliwa 2 months later, nikakaa kama miezi 6 nikaja kumpaja mume wangu huyu nae kapigika kimaisha kweli kweli kila mwanamke anamkataa tokana na hali yake ya maisha ni duni, aliponiona tu hakunitazama mara 2, akajua ndo wanawake wale wale wakishua, basi tukafanya biashara pale na nini, kwa muda wa miez 2 akaniona wa tofauti kwakweli, akanipenda akaja kunitongoza miezi 6 baada ya kufahamiana, tukaanza mahusiano ndani ya miezi 2 akapropose, akataka kutoa mahari nikamwelezea kuhusu prenap akasema haina neno nishapenda tenaa akasaini ndani ya mwezi m1 mahari, sendoff mwezi wa pili yaani mwezi wa 8 tangu kufahamiana nikaozwa sharehe kubwaaajee, marafiki wa mzee kibaoo, mawaziri, wabungee, diwani, waziri mkuu, meya wa Dsm yani harusi ya watu 300 nikaozwaa, baada ya miezi 9 nikajifungua mtoto wa kiume, mtoto wangu nampenda sana
Jembe langu la nguvuu nikampeleka kwa baba yangu mzazi, akamshikaa, akampendaa akaomba aitwe jina lake mume akakubali .. Babu yake akamwombea mwanangu wee mpaka mwisho akaguna mmh.. Akakemea mauti. Sikuelewi kwanini aliomba maombi yake lkn tangu mtoto amefariki sasa namwelewa kabisa babangu alivyoomba..

Gigi bwana ana ujinga kidogo yule mkwe wangu, mimi nilikataa katu katu mwanangu asimuoeeee kwanza kabisa mwanangu ni mdogo kwa Gigi kwa miaka 2, sasa Gigi na ukubwa ule si ananibemendea tu my son, basi marehemu mwanangu akalalamiiika kweli kweli mama nampenda and stuff dah basi nikamkubalia sawa muoe, lakini ndoa yenyewe ikawa inaenda kumagumashije sasa, kama nilivyo predict, mwisho wa siku mwanangu my only son akafaaa hakuna kitu kinauma kama hicho afu mwisho wa siku unaskia mkweo aliolewa na mwanao kwa ajili ya revenge ya marehemu ambae anadhania me nimemwuua! Kha hapana asee!

Nilichoka na kuchoka nakuchokagaaa!
Nakuwaje muuaji wakati me na babake ni wapenz?!

Unajua ngoja niache kuongelea swala la marehemu baba Gigi labda siku nyingine maana kuna kesi inaendelea mahakamani labda huko ndio watanielewa..

Kuhusu mume wangu sasa baada ya kumzalia watoto wa 3 akaelewa biashara ilivyo na jinsi ya kutoboa akajisahauu.. Mara alale na ndugu zangu, mara alale na maids, mara alale na wanafunzi ifm, udsm, cbe, eh mume keshasahau prenap inasemaje, nikasubiri nimalize uzazi wa bongee, nikakaa mwaka nikafukua makaburi yangu ya misri, yeye akiwa na affairs zake am having mine, Mimi na baba Gigi tukarudisha mapenz kama kawa, mkewe hajui, tunajifungia bgamoyo, kigamboni, arusha nikampa cheo finance manager ktk kampuni zangu zotee, mkewe alipojua tuka stop kwa mwaka m1, kwan vepee?

Mwisho wa siku am holding the fort, on my high horses, kwa raha zangu, mwenye hela mimi, prenap inanilinda mimi na watoto na wajukju na vitukuu vyangu..

Huyu mume nishawahi kumfumania na house maid kitandani kwangu, mume hakujua kuwa nilishawekaga cctv camera toom nikachukua evidence nikapelekwa kwa lawyer wangu wa prenap akaniambia siku yeyotr utakayokuwa tayar kuomba talaka prenap inakulindaaaaa! Sasa hivi naweza mwacha huyu pimbi mume bila kitu maana spend manyanyaso ... show yangu kwake imeshaisha muda kanipa watoto kwenye ndoa asiniumiza kichwa

Sasa Tausi asidhani atapata maisha yale yale watarudi from scratch na huyu pimbi husband wangu we waache tuu.. hapa nikimdaka tu na Tausi wana do na record napeleka kwa lawyer nadai talaka nile uzee wangu kwa nafasi hapa nilipo sina ukimwi limume liniletee aku staki
Niliwafundisha vzuri sana watoto wangu na wakanielewa kuhusu prenap.. Hata
Mume wa dadake bonge, my son inlaw alikubali ku saini, baada ya hapo ikawa zamu ya bonge akafail kupata mumee nikaona hapa lazima ni play my cards right la sivyo mali zitapoteaa

Mark wiki 2 kabla ya harusi nilimweka sawa, nikamwambia skiliza we tuyuu, nakupa mwanangu muoane hautajutaa, nakubadilishia maisha mpaka unakufa hautataabika, nikamwonyesha mali na prenap na kila kitu akatamaani, maana maisha yangu ni 1st class na high end stuff, nilimwona sana machoni alivyojaa tamaa, nikajua atarudi ingawa aliniomba muda afikirie baada ya wiki akakubaliana na ishu yangu, nikamtambulisha kwa bonge mwanangu kumbe walishafahamianaParis, ndio ivyo wakaoana, sasa roho yangu imetuliaa, kijiti cha kizazi cha 3 hakinihusu kabisaa nimeshamaliza kwangu naweza

Lala na baba zangu kwa amani zote kijiti cha utajiri nimeachia warembo wangu wakipeleke mbele i hope watafanikiwaaa

Sasa wewe Mtz ongea unavyotaka mpaka mwisho, am living large, maisha hayatakaa yashukee, hakuna nchi sijasafiri, sijawahi lala njaa, sijawahi kuwa na kiu ya dyudyu nisikidhi kiu yangu, hata nikifa Mungu lazima anireward na Gold Crown.
Kwaiyo mtajiju,
Mimi ndio mama Bonge
On my high horses"




TUONANE TAR 17 MARCH 2018 SAA 1 USIKU YA TANZANIA

________________________________

E. GIGI THE BADDEST




Ahahahahahhahahahahaha

Uuuuuuuwiiii

ahahahahahahahahahahahahahahahahaha

we mzee wewe ni noumer sijawahi kuonaaaa
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Ahahahahahahahahaha

Dah hii ni kali ya mwaka



Gigi: we mzee ni mafiaaaa akyanani me skujua kama unamjua huyu mama kiasi hichoo



Mzee mlinzi: yap namfaham sana sana sana ila yeye hanikumbuki



Unajua huyu Eva amenisahau au anajifanya hata sielewi baada ya kumsaidia Mama Bonge,

Babake mzazi akaniambia niangalizie binti yangu ila yule mzee unajua kama mwanga gigi

Hii siri yake ya familia lazima niipelekeee mahakaman kama ilivyo yule mzee nimemwota miezi 6 kila siku mfululizo ananiambia ahadi yangu haujaitimiza fanya haraka hauna siku nyingi



Gigi hapa tunaweza gombana kabisaa hii mimi staki kufa najiona



Gigi: oi mzee ujue nimekutoa uswazi sa mbona unanikimbia



Mzee mlinzi: unajua Gigi hivi vitu vingine niliapa agano la damu sasa unajua mambo ya mila hayanyakuliwi kwa pesaa we niache kwanza nikamilishe nilale kwa amani sina rahaaa



Gigi: mimi nataka kumnyoosha mama bonge wewe unaleta za kuleta sio?!

Ntakuuua mzee wewe haunijui ee



Wakaanza kugombana hapo weee mpaka wakaanza kupiganaaa mzee mlinzi akashikwa kooo hapooo akawa ana fight kukabwaaa anatoa mimachoooo anakata roho Gigi kamkaza kweli kweli

Baada ya muda mzee mlinzi akashtuka usingizini



Akaanza kuhema juu juu akanywa maji kama ngamia alietembea jangwani akakaaa anawaza na kuwazua na kifikiriaaaa, huyu mtoto nisipojipanga ataniua kweli na hii ndoto ni warning asee kwa babake mama bongeee Eva.

Dah sasa hapa niende sawa

Na gigi lkn niwe na macho 4 ya ziadaaaaa

Ndio anenitoa uswazi lkn uswazi kwenyewe nilienda kujifichaa nikijua mama bongee hawezi nipataaa sasa kukaa uzunguni huku bunju nako ni balaa tupu



Akaanza kutunga sheria saa 11 asbh mpaka saa 3 anachora tu maraman akawa amejikalia barazani kwake mara anaskia honi ya gari

Akaenda mlinzi akalifungua geti kumbe ni gigi



Mzee mlinzi: karibu mama za masiku sijakuona miezi 3 sasa



Gigi: naendelea vzuri baba za kwako?! Za kushinda baba?!



Mzee mlinzi: salama mama nipo tu

Ile kazi yako kwa mama bonge nimeshaimalizaaaa na ameshampa talaka mumewe wamegawana mali nusu kwa nusuuu



Gigi: akafurahia hapo anapiga vigelegele alililililililili

Uuuwi haleluyah kweli Mungu yupo



Mzee mlinzi anamwangalia anaumia roho kweli kweli



Gigi: ngoja nipige kwanza simu nihakikisheee



Phone: haloo Aaliyah embu nipe news



Aaliyah: baba bonge yupo single mamaa he is a free agent darling



Gigi: kweli?! Lini imetokea



Aaliyah: majuzi tu hapa wame reconsile na mali wamegawana nusu kwa nusu walizochuma baada ya ndoaa


ITAENDELEA

About THE STORY BOOK

0 Comments:

Post a Comment