Chombezo : On My High Horses
Sehemu Ya Kwanza (1)
CHAPTER 1
A. MWANZO MGUMU
" Siamini kama Mark kamuoa lile bonge malaya .. how could he?!, baada ya mambo yote tuliopitia jamani ameamua kumchagua yule bonge?!That sun of a bit**",
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
huku anagonga meza, kwanza
Mwanamke mwenyewe amekaa kama michellin jaman! Hana kiuno hana shingo yani shapeless
Sio haki kabisa, Maisha hayatoi haki kabisa!
Kwanini Mungu kwaniniiiiiii?!
Mimi sio mtu mbaya ujue Mungu?!
Mimi mbona nakupenda sana kwanini umeamua kunitesa namna hii?
OMG! Huku analia, mama yake anambembeleza
Mama: basi mwanangu acha tu huenda hakuwa wa kwako Mungu amekuepushia
Aaliyah: Mungu asingeruhusu tukae miaka 9 kwenye mahusiano kama hakutaka niwe nae, sijawahi hata kumfuania Mark kwa sms, simu, picha, inbox za social medias,sasa imekuwaje!?
Au amelogwa na huyo michellini?!
sio fare mama, not fare at all, huku analia kama chizi amejilaza kwenye kitanda chake
Mama: akawa anambembeleza tu hush hush mwanangu, akapanda kitandani akamkumbatia, wote wakawa wanalia, mama anambembeleza mwanae"
Lakini miaka 9 mingi jaman!
Yani unamwacha mwanaume anakuburuza mwaka 1 ... 2.... 3.... 4.... 5.... 6....7...8 ....9 alafu anakuja kuoaaa ndani ya miezi michache khaaa!
Wanawake sisi tumeumbwa kipekee sio kitoto... kama Mbinguni kuna special previlage basi wanawake wanachukua gold medal
Embu mimi Penny nisiwe mbea sana niendelee na stori yetu
Miezi 2 kabla ya harusi
A. PARIS
Mark:
Mpenzi nakupenda sana, nakupenda kuliko neno nakupenda lilivyo, nakupenda to the moon and back, mapenzi yangu kwako nimefika on cloud 9, nakupenda to infinity
Aaliyah:
I love you too darling, you are the best thing ever happen to me, 9yrs ni kama nimekufahamu jana, mapenz yangu kwako hayachujuki wala kufubaa wala kuoza wala kunuka wala kuchachaa, wewe ni halichachi wangu! You are my forever best friend
Waka kiss kiss kiss ika turn into romance romance turn into mechi kwenye balcony ya chumba chao nchi ya Paris
Na ahadi za mechini si unazijua tena game likikoleaaaa, mwanaume anatoa ahadi kibaaaaaooo i will never leave you or forsake you, your my hero i love you forever, i will marry you!
Aaliyah akaidaka kichwani akijua soon njema Mark ata propose maana ishakuwa
9yrs tena, mapenz yao yalianza high school mpaka chuo wakamaliza mpaka wameanza na kazi wamekuwa promoted wapo kama bolt na nati, hawaachani wakaamua kuchukua vacation pamoja kwenda Paris,
Wakakaa wiki 2 Mark hana dalili ya ku proposeee, kama ni surprise basi Mark anatoa surprise za maua mekundu, meupee labda anamdanganyia na diamond rings au neckless au barcelet au watches za bei ghali lakini hakuna ring!
Aaliyah akawa ameshaanza kuwa na wasiwasi huenda amezeeka au Mark amemchookaaa hata hakuelewa kuna shida gani
Aaliyah:
Mark is a huge successfull man in Tz, kinachomfanya asioe ni nini?!me nimekaa nae miaka 9 sijawahi hata kumfumania kwa sms wala simu wala live akiwa na mwanamke mwengine,
Sidhani kama ana uhuni wa kijinga sidhani pia kama ni ****** maana dozi nazopewa sio za kitoto kila siku nabadilishiwa mastaili
Kwanini lakini Kwanini hanioi?!
Nina miaka 30 sasa, marafiki zangu woooote wameshaolewa na wana watoto wa 2, mimi tuuuu jaman au nimelogwa mbona nasali sana jamani, a committed church member wapi nakosea?!
Sijawahi hata kumtukana huyu mwanaume tusi lolote tangu nimemfahamu hajawahi kuniskia nimemwita mjinga, mshenz, fala, pumbavu, ****** yani hata kumsonya hajawahi kuskia nikinuna nikikasirika nazima simu taratibu nalala kitandani nalia weee hasira ziiishe lakini sasa nahisi nitakufaaa nahisi kupasukaaa volcano yangu inataka ku-erupt, siwezi jamani,
Ila sasa kasema anataka kunioa labda ni kweli ngoja nivumilie
aaliyah anawaza hayo wakati Mark anampiga mechi... mwe mwanamke kwa kufekisha badala ya kuskia utamu anawaza kwanini haolewi?! Kiru!
Siku moja wapo njiani wanazunguka madukani Paris wanafanya shoping.. wakaingia kwenye duka moja wakapishana na demu m1 bongeeee mweusiii shapelesss yani michellin atasubiria sana, wakaingia zao ndani ila Mark alikuwa na jicho la 3 kuhusu huyo demu
Mark:
Duuh huyu dada bonge sana, kha!
Kazi ipo mwanamke kama yule si afanye tu mazoezi aende gym unene ule mbaya sana mpenz
Aaliyah:
yah nimemuona maskini probably anaumwaa!, ah tuachane na hayo mpenz tuendelee na ya kwetu sawa darling?!
Mark:
sawa! Huku anamwangalia yule bonge anavyoishia
Baada ya wiki 1 wapendanao wakarudi Tz, kuendelea na kazi na maisha
All lovey dovey mubashara kwenda mbele, mapenz yakaongezeka hamna alieonekana amepunguza mapenz kwa mwenzake
Mwezi 1 kabla ya Harusi
Tausi:
darling, next month kuna harusi ya rafkiangu anaolewaaa! Naomba unisundikizee
Aaliyah:
ah naji huyo tena maana isije ukawa unaolewa wewe
Tausi:
ah shogangu mimi bado sana ngoja nile kwanza ujana, kuna shogangu m1 huyo bwana kani surprise ni boooonge la booongeeee!
Yani bongeee sijui nikufananishie nini eti kapata bwana mwezi uliopita walikutana huko Paris
Aaliyah:
ah! Okay hongera zao Paris a city of love she's lucky!
Tausi:
Basi bwana akaniambia huyo kaka walikutana kwenye duka la nguo then bdae wakaja kukutana tena night club!
Wakasalimiana wakanywaa wakalaa wakaenda mziki wakachezaaa wakanywaaaa wakanywaaa mpakaaaa kuja kushtuka asbh hawana nguo wapo kwenye chumba cha shogangu walisha du zaman tena bila condom!
Eh! Basi yule kaka akaaga anasema mama yake yupo hospital anaenda kumwona akaondoka hata hawajapeana mawasilianooo!
Hawakuonana tena mpaka waliporudi tz wakaja kukutana bank, hapo Crdb holland house posta mpya, wakasalimiana wanakumbukana wakabadilishana no!
Tangu pale ni mechi za hapa na pale bila kinga
Aaliyah:
bila kinga?! kha!
Huyu bonge anajipenda au ndo desperation?
Tausi:
mimi nilimwuliza swali hilo hilo akasema yule bwana alimwambia condom ya nini?!
Bonge akakomaaa wakaenda kupima wote hawana wakaona waendeleze kavu kavu, kavu ikawa kavu mpaka bonge akapata mimba hapa nakeambia bonge ana mimba ya miezi 2, mwanaume amechanganyikiwaa
Kusikia bonge ana mimba
... wiki 3 zilizopita huyo bwana akamwita bonge Kempinski akamnunulia lunch zile za j2 after church wanaziitaje sijui wamemaliza kula mwanaume ana propose waaaaa, will u marry me, bonge hakuaminiii! Akaona fairy tale imemuangukiaaa gadame!
Akafurahi basi kulikuwa na band inapigwa pale ni full nderemo na vifijooo!
Bonge ndio akawa proposed kavishwa pete matataaaa, zile pete za Diamond zenye karat 7!
Nomaaa!
Aaliyah:
kha! Nomaa!
Bonge ana bahati balaaa! Tena iyo pete naipendaje sasa?!
Uuuwi i wish ningekuwa yeye jamaan
Tausi:
ndo ivyo next month harusi tena ya watu wachache kama 30 tu wazazi wa mwanaume na mwanamke na marafiki wa karibu, bkoz bonge hataki azae anataka watoto wazaliwe ndani ya ndoaaa! ila me bestito nimepewa card 2 naomba plz plz plz unisindikizeee
Aaliyah:
ok u just keep me posted week 1 kabla nitakusindikizaaa nikaone iyo fairy tale wedding..
wakaongea weee baadae kila mtu akajikataa kivyake!
Usiku Mark akakutana na mpenz wake Aaliyah
Mark:
babe kesho nasafiri kikazi naenda Arusha, kuna kikao na mkurugenz wetu na shareholders wa kampuni yetu, kurudi baada ya week 3,
Nimeskia tetesi wanataka kunifanya partner wa kampuni yao, nahisi bonus na mshahara vitapanda na kila kitu!
Bonus napewa nyumba, gari, fuel, 13th cheque kama kawa na kama nitapata watoto watasomeshwa UK, so we better hurry up kwenye kupata watoto i think we should get married
Aaliyah:
oh jaman! hongera sana na mabusu kibaooo!
Nadhani inabidi tuoane sasa!
sasa mimi ofisini nimebanwa sasa hivi nikipata nafasi nitachomoka weekend moja nije kukuona!
I love you!
Mark:
i love you more!
Aaliyah:
hongera sana sana sana i envy u
SIKU YA HARUSI:
Mark:
amefurahi yupo saloon na best man wake na best friend wake
Best friend akamvuta mark pembeni, we Mark unamwoa nani tena?! Aaliyah a?
Mark:
sssshhhhh! Nooo not Aaaliyah! Kuna demu mmoja bonge ndIo namuoaaa!
Best friend:
kivipi?! imekuwaje tena na Aaliyah?!
Mark:
shit went down akaondokaaa!
Na unajua no man is an island i was drunk my ass off nikaja kukutana na huyu baby mama wangu tukalala,
ilikuwa one night stand ambayo ili turn into pregnancy!
(kama haujui mpenzi msomaji, Mark ni Proffessional lier ila twende nae mdogo mdogo tuone mbio zake zinaishia wapi)
Best friend:
oh my God!
Sasa Aaliyah anajua unaoa leo?!
Mark:
hajui maana alikataa nisiwasiliana nae
Best friend:
something is not right but hey! Ni maisha yako haya! You did the right thing kwa kumuoa huyu dada mlee sasa watoto hongera, unakuwa baba soon ndicho ambacho ulikuwa unakitaka siku zote!
Mark:
namshukuru Mungu kwakweli
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Best Friend:
i hope your right but bado sina amani na hili dwala la Aaliyah!
Sijui kwanini roho yangu inaniuma sana tangu umeniambia haumuoi aaliyah nyie watu mmetoka mbali sana mnajua?!
9yrs haiwezi kutupwa kapuni kirahisi namna hii
Mark:
relax man Aaliyah nimemvumilia sana ila i nahisi ni Mungu alizuia sasa sijui bwana nimechoka
Best friend:
du! Haya bwana kama umeamua hivyo me siwezi kukuingilia wala kukuzuilia, your happiness counts!
Hongera sana kwa mtoto ana miezi mingapi shemej
Mark:
2 tu
Best friend:
mmmh hongera sana, haya vaa hili koti tuwahi kanisani
Harusi ikafungwaaaa!
Officially Mr and Mrs Mark!
Watu kanisani wapo 15 tu wakajongea ukumbini Double Tree hill by Hilton Oysterbay Dar es Salaam!
Sherehe ikaanza wageni waalikwa wakaingiaaa wamependezajeee executive 1st class wedding!
Ilipendezaje wapiga picha kibaoooo makamera makubwaaa kama ya BBC!
Tausi na Aaliyah wakaingiaaa dah harusi nzuri hiooo
Wakakaribishwa wakakaa nyuma nyima si unajua masista duu tena hawapeend kukaa mbele kama wachungaji.. wao wanazum tu toka nyuma!
Baada ya nusu saa maharusi wakaingia ndani, Mc akawakaribisha ikabidi wasimame, maharusi wanaingia
Aaliyah akapigiwa simu na mama yake, akageuka pembeni maharusi wakapitaaa hakuwaonaaa, walipopita yeye akatoka nje kuskiliza simu, akamwambia Tausi nakuja mama amenipigiaaa
Akaenda kuongea na simu mvua inanyeshaaaajeee sasa hawasikilizani
Mama kwenye simu:
uko wapi mwanangu
Aaliyah:
nipo kwenye harusi ya rafkiake Tausi hapa Double Tree hill by Hilton
Mama kwenye simu:
mami ondoka hapo tafadhali
Aaliyah:
mama sikuskii unakatika katika jama mtandao naonaa unasumbuaaa
Mama kwenye simu:
hunny ondoka hapo rudi nyumbani
Aaliyah:
niondoke kuna nini tena mama?!
Mama kwenye simu:
Mark anaoa leo haujaskia
Aaliyah:
mama skuskii jamaa unakatika katika, Mark kafanyaje? Halooo halooo halooo
Mama kwenye simu:
Mark anaoa leo anaoa hapo hapo double tree hill ondoka hapo, tafadhali njoo nyumbani, umeskia mwanangu?!
Haloo ...halooo ...haloo ...akaangalia simu imeshakataa
Aaliyah:
ah mama nae! msumbufu simu yangu ishazima hata sijamwelewa anasema mark sijui kafanyaje embu ngoja nikamuazime simu
Tausi nimpigie
Akarudi ndani anakuta watu wanachezaa mziki na maharusii!
Kumcheki Tausi yupo mbele anaserebukaje mziki wa diamond platnums!
Akakaa kwenye kiti ila roho inamsukuma aende mbele akachezeeee!
Akachukua pochi yake akamfuata Tausi kufika anamkuta Tausi anacheza na Bonge akimwangalia vizuri sura ya bonge sio ngeni kwake akamfuataaaa Tausi,
Tausi:
eh bora umekuja nikutambulishe rafkiangu Bongee wakasalimiana pale
Aaliyah:
hongera sana harusi yako nzuri mno umependeza sana!
Bonge:
asante sana, oh My husband huyu hapa ngoja awasalimie kabla hamjakaa Mark njoo
Mark akaja buana
Bonge:
jaman huyu ndio mume wangu Mark!
Aaliyah:
kumwona ni Mark, akashtukaaa kama amepigwa risasi kifuani!
Akahisi miguu imekufa ganzi akamshikilia tausi akapata na kichefuchefu akawa anataka kutapika akajizuiaaa
Mark:
makavuuuu mkavuuu usoni akawasalimia mambo warembo salama?!
Tausi:
salama shemeji hongera sana, mmependeza sana
Mark:
asante sana
Tausi:
shemeji huyu rafkiangu anaitwa Aaliyah
Mark:
oh! Mambo Aaliyah?! Akampa mkono!
Aaliyah:
akatoa mkono mdomoni ampe Mark akamtapikia buuuuuuuwaaaaah! Kwenye suti yake, akazidi kutapika Tausi akaomba radhi akamwondoa akampeleka kukaa
Aaliyah aliliaaaa, aliliaaaaa wageni wanamshangaa ikabidi Tausi amtoe ampeleke nje ya holi akakaa nae reception analiaaa Tausi haelewi analia nini!
Bonge anashangaa imekuwjae tena, huku anamsafisha suit mumewe akaja best friend wa Mark akamchukua Mark mpaka washroom
Best friend:
imekuwaje mzee mbona aaliyah kaja?!
Mark:
amepaniki hata sijui
Sijui nani kamtonya au yule demu Tausi?!
Best Friend:
kwani unamjua Tausi
Mark:
hapana nimetambulishwa yule Tausi na mke wangu Bongee ni rafkiake sana
Best friend:
sasa utafanyaje?!
U have to play cool kama haujaona kitu au haujui kitu ngoja niende kumcheki Aaliyah nje niongee nae mara akaingia bi harusi
Bonge:
are you alright mume wangu? Huku anampulizia perfume kwenye shati koti akalitoa akamvalisha lengine
Mark:
am fine darling asante sana wakaondoka haooo mpaka kwenye sherehe
Tausi:
sasa Aaliyah unalia kisa umemtapikia bwana harusi embu acha utoto na wewe
Aaliyah:
plz naomba niache kwanza we nenda kwenye sherehe nipate upepo kwanza then ntakucheki tuondoke ok
Tausi akarudi ndani akameacha Aaliyah yupo nje analia na kujifuta machozii
Mara akatokea best friend wa Mark
Best friend:
Aaliyah!
Aaliyah:
akamwangaliaaaaa akawa analia
Best friend akaenda kumkumbatia Aaliyah, maskini aaliyah analiaaa haelewi anaona kama ni ndotoooo!
Why why jaman Mark amenifanyia hivi jaman amenidanganya anaenda kikaz arusha kumbe anaoa?
Kama sio Mungu mimi nisingekuja hapa huyu Tausi ameniomba sana nimsindikize ila leo njiani wakati nakuja roho inaniuma sana sikumwambia tu nikaona nimemuahidi namsindikiza ndio nakutana na haya
Akajinyofoa kwa Best friend akamzaba kibao
Aaliyah:
ulijua kuwa anaoa sio?!
Best friend:
hapana mimi kaniambia jana njoo naoa hata sikuuliza nikajua anakuoa wewe kuja ananimbia leo anaoa mtu mwengine nikakupandia hewani haupooo nikaamua kumpigia mama yako kumweleza kwani hajakwambia mama yako?!
Aaliyah:
oh my gaaaaad! Amenipigia tukawa hatuelewani maskini! Nilikuwa nimeshafika ukumbini ila sikumwona Mark wakati wanaingia
Nitafanyaje sasa mimi, miaka 9 ya mahusiano na Mark anaishia kumuoa mtu ndani ya miezi 3
Best friend:
ameniambia ni mjamzitooo!
Aaliyah:
kwaiyo hajanioa mini kwasababu sijamzalia au?! Angekuwa na shida ya mtoto si angeniambia me nameza mavidonge najilinda jaman wanaume jamaaan me hata sijui nawafanyaje huku analia
Best friend nae yumoooo, eeeh! Kesi ya nyani best friend anakumbatiaaa tuuuu! Aaliyah analiaaaaa analiaaaa kwenye kifua cha best friend
Best friend:
aaliyah mama we nyamaza naomba nikurudishe nyumbani tafadhali, tuondokeee wakaondoka haooo
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Njia nzima aaliyah analiaaa Best friend ameongea maneno mazuri ya busaraaa ya kumtia moyooo ya kiMunguuu lakini aaliyah hakuwepo ulimwengu huu wa duniaaa hiii, alikuwa ahera kama sio Mbinguni kwaiyo hata hakuskia Best friend ameongea nini!
Kufika nyumbani akamshusha mama aaliyah akaja kumchukua mwanae kwenye gari mvua inanyeshaaa mama katoka bila mwamvuliiii, anambembeleza mtoto wanatembea huku wanalowanaaa best friend anaskitika lkn atafanyaje akarudi zake ukumbini akamwambia Tausi Aaliyah nimeshamrudisha kwao alikuwa analia sana so usimtafute, best friend akaendelea na sherehe ya Mark na Bongeee
Aaliyah:
jaman me hata siamini Mama siamini kabisaaa
Aalafu bi harusi mwenyewe mama tulikutanaga nae Paris kibooonge shapeless, akawa anamsema vbaya kumbe wanajuana i bet hata kuja paris alikuwa amemlipia uuuwi mama nitaenda wap na miaka yangu 30 nimekataa wanaume wooote for Mark Mama hata sijui nafanyaje sijui nitaenda wapi?!
Siamini Mark kamuoa yule changudoa .. how could he?!, kwa yote tuliopitia kamchagua yule bonge?
Malaya mkubwa yule, huku anagonga meza, kwanza
Mwanamke mwenyewe amekaa kama michellin jaman! Hana kiuno hana shingo yani shapeless
sio haki, maisha hayatendi haki! Kwanini Mungu, kwanini?!
Mimi sio mtu mbaya ujue Mungu?! Mimi mbona nakupenda sana kwanini umeniamua kunitesa namna hii?
OMG!
Huku analia, mama yake anambembeleza
Mama:
basi mwanangu acha tu huenda hakuwa wa kwako Mungu amekuepushia
Aaliyah:
Mungu asingeruhusu tukae miaka 9 kwenye mahusiano kama hakutaka niwe nae, sijawahi hata kumfuania Mark kwa sms, simu, picha, inbox za social medias, sasa imekuwaje!?
Au amelogwa na huyo michellini?!
hii sio haki kabisa mama, sio haki huku analia kama chizi amejilaza kwenye kitanda chake
Mama:
akawa anambembeleza tu hush hush my daughter, akapanda kitandani akamkumbatia, wote wakawa wanalia mama anambembeleza mwanae ...
TUONANE TAR 26 FEBRUARY 2018 SAA 10 JIONI YA TANZANIA!
_____________________________________
B. ALCOHOLIC MEETING
Ok karibuni sana, mimi naitwa Doctor Grace, nimesomea PHD in psychology
Watu:
muaaaah, aaaaammmm, (wanapiga miayooo)
Doctor Grace:
awkaaay! Tuanze kikao chetu maana naona mshachoka
Kikao tutafanya kila j4 saa 5 asbh mpaka saa 7 mchana na alhamisi saa 1 jioni mpaka saa 3 usiku sawa?!
Watu:
sawaaaa, poaaaa, whatever, oh shit, that's dope, okie dokie maam, aina noma dokta, barida mama kubwa bariiiidaaaa!
Doctor Grace:
napenda kuwakaribishwa wageni wapya kwenye kikao chetu, kikao chetu kinaitwa STRONGER, maana sisi ni stronger sisi sio looser kama wanavutuitaaa
Nakaribisha wagen wapya naelewa kuna Aaliyah na Zoba na Mbovu na gumegume, karibuni sana
Haya leo tuanze na nani kati ya nyie wagen tuwaskie nini kimewasibu mkaja hapa kwenye hizi Alcoholic Meetings
Aaliyah:
Love!
Doctor Grace:
Love imefanyaje tena?
Aaliyah:
Love changed my life, Pain hanged me
Nikaanza kunywa pombe wakati sijawahi kunywa pombe tangu kuzaliwa kwangu, me nimeokoka nampenda sana Mungu
Wagonjwa:
ohoooo, fcku, Jesus Freak is here, uuuwi mlokole kapinduliwaaa, ahahahahaha wote wakacheka
Dr Grace:
aaaaah jaman naomba tukae kimya huyu ni mgeni hamna kuchekanaa... enhe Aaliyah endelea
Aaliyah:
well ndo ivyo tangu mimeanza kunywa pombe wazazi wakaona nije huku kabla sijapoteza ajira ... anyway naomba niishie hapa kwa leo aongee mwengine huenda nitapata nguvu ya kuongea muda ukibaki au siku nyingine
Dr Grace:
asante Aaliyah umefanya vizuri sana, enhe nani anataka kuendelea ambae ni mwenyeji?! Nani?!
Ili wenyeji wasipate woga wa kuongea nani anataka kuongea leo tumsikilize?!
Gigi:
well doctor leo kidogo nina nguvu naweza kuongea
Doctor Grace:
karibu Gigi, karibu sana haya tumsikilize Gigi jaman anataka kuongea, wanasema sharing inasaidia ku release anger na stress na kuondoa sumu katika maisha yetu, karibu sana Gigi
Gigi:
hi am gigi and am an alcoholic
Wagonjwa:
hi Gigi, tsup babe, uuuuuwiiii gigi my baby, pheeeewww pheeeweeeew!, toto gigi hilooo, tupe vyombo gigi, basi kila mtu anaitika kivyake!
Gigi akacheka: anyway ngoja nianze kwanza namna hii
Mimi sio alcoholic, nakunywaga tu pombe ku release the anger
Doctor Grace:
lakini repost imekuja toka ubalozi wa marekano imesema wewe ni mlevi na kama unataka kukaa kazini lazima uwe sober ndio maa a upo hapa
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Gigi:
bitch fcku that report! Am clean, cleaner thank you all
Mgonjwa m1:
i know baby, ndio maana me nawewe tukitoka hapa lazima tukapunyuane u know what am saayiiing (huku anamkonyeza)
Doctor Grace:
jaman tutulie jamaa mnapoteza muda, kumbuka ukitaka kupona na kurudishiwa maisha lazima uwe serious, u pay attention, bila kutulia sitakuandikia report nzuri nanhautarudi kwa familia au maisha yako uliokuwa unaishi
Wewe Kibovu una mtoto anakusubiri
Kibovu:
mmmh! Ilo nalo neno
Dr Grace:
we gumegume mamako anaumwa hoi so pona haraka ukamwone la sivyo hauwezi kutoka humu hospital
Gumegume:
doctor basi usinitoneshe kidonda doctor plz
Dr Grace:
na wewe Zoba kiongozi wa fujo nitakufukuza urudi jela
Zoba:
ah madam weee jela nikafirwee
Bora tu nikae hapa jamaa nikimwona Gigi na Aaliyah me mbona salama tu hata kama ntadinda kuliko ku***** bora nidinde
Dr Grace:
ndo ivyo utulie tena nyie niliowataja mpo kwenye hali mbaya bora hawa wenzeni akina Aaliyah na Gigi wanalala makwao plz naomba utulivu
Wagonjwa:
barida dokta, sawa tu mamangu, poa endelea madam
Dr Grace:
haya gigi endelea tafadhali
Gigi:
well like i said me nipo clean nina imani hiyo kama hamtaki kuamini basi me sina haja ya kuwalazimisha mniamini
Dr Grace:
kwanini unasema upoa clean, kwani ulikuwaje kabla haujawa clean, nini kilikupata mpaka ukaanza kunywa sana pombe na ukaua mume wako?
Gigi:
mIMI sijaua mume wangu alikufa mwenyewe
Dr Grace:
report imesema umeua
Gigi:
Dr tuheshimiane soma vizuri report hapo chini, mama mkwe ndo alisema nimemwuua mwanaeee ila mimi sijauaa according to the cctv cameras zilionyesha alikufa mwenyewe kea heart attack na hakuwa na mtu wa kumsaidia
Dr Grace:
oh yah! imeandikwa hapa
So tuambie gigi ikawaje ukawa mlevi wa kupindukia mfanya kazi mzuri wa ubalozi wa marekani?!
Gigi:
well hata sijui nianzie wapi ila poa tu kama utanielewa shega kama haunielewi barida tuuu mama lake
Wananiitaga a lady gwithout a soul, nina miaka 32, widow, now nipo jobless kwa muda mpaka nitakapopona hapa, but my lifestyle ni kama mtu ambae amekaa kazini miaka 10.
Kazi ya ubalozini nimeipata 1yr ago baada ya kutengana na mumewangu kabla ya mume kufariki, ila mama mkwe na hela zake akaja kunibamiza ofsini kisa ana hela na nini kanichomeeea nisafe
Gigi:
mimi kwetu nilizaliwa pekeyangu, mtoto wa kike pekee baba yangu alifariki nikiwa mdogo kama na miaka 20 kwa ajali alikuwa anafanya kazi ofisi ya mama mkwe wangu kama mhasibu
Ila najua tu walimuuua, maana yule mama mkwe mshenz kabisa kitombi balaa just bkoz ana hela haimaanishi awe anatembea na wafanyakazi wake hamuheshimu hata mumewe ila poa tuuu me naongea tuu
Doctor Grace:
Gigi unajua haya maongezi yanarekodiwa sio?!
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Gigi:
wala sijali hata mkirusha ITV poa we mama mkwe umeniuliza baba yangu ****** kabisa
Muda huo babangu anafariki me nilikuwa nasoma UK degree ya kwanza, nipo mwaka wa 2, mimi nipo smart sana nimeanza shule nursery nikiwa na miaka 3, nimemaliza form 6 nina miaka 16, chuo nimeanza nina miaka 17 by the time nina miaka 20 nipo chuo mwaka wa 1 maana UK walisema me mdogo sana wakanipeleka diploma miaka 2 so by age of 20 nipo uni mwaka wa 1
Kuja kuambiwa baba yangu amekufa nililia sana, si unajua baba yangu ndo kila kitu ndio my 1st love ndio kila kitu, alikuwa best friend wangu kinyamaaa nampenda sana marehemu babangu
Naja kuambiwa aliesababisha kifo chake ni mama mkwe sikuelewa elewa mpaka nilipograduate chuo nikiwa na miaka 22, nilisomea sheria (law)
Uzuri mama alikuwa na kazi yake PPF aka make sure na zile life insurance masoma namalizapaka napata bar nakuwa lawyear nina miaka 23, sijawahi kufeli, kusapua, kilaza, me nikiingia class nikiskiliza lecturer tu basi hakuna mtihani unanipita mambo ya zima moto sijui me nikuattend darasa na kupasua sijawahi kushuka A+
Nimegraduate degree na 1st class, nikapiga bar nikapataaa,
Nikarudi Tz kuomba kazi wakati visa ya UK haija expire
Kurudi mama mkwe akaskia nimemaliza nadhani mama alimwambia akamwomba nifanye kazi kwenye kampuni yake, maana hawakuwa na lawyer mzuri sana,
Mama akaniomba ingawa sikutakaa maana walimwuua baba yangu, but mama akanisihi amaana kazi zilikuwa hamnaga kipindi hicho nikaenda na akilioja tu ni investigate what happen kwa baba yangu na kwa nini alikufa kifo cha mendee?!
Siamini mpaka leo na sijui kwanini ky 1st love alikufa.. nilienda pale kwa mission moja tu kujua kwanini baba yangu alikufa tena kafia ofisini kwake?
Nikaongea na lile li mama mkwe tukakubaliana mshahara akawa ananilipa kwa pound maana nilimwambia me nina kazi nimepewa UK so kunichomoa inabidi unilipe kwa same amount na same currency akakubali si mashauzi ana helaaa!
Nikaanza kazi mwezi wa 1 ... 2....3 kakaja kamwanae kakiumee! Kalikuwa kanaishi marekani kamekuja kusimamia family business kakaanza kunifukuzia me wala simtaki sikumpenda sio kwamba nilikuwa na beibe hapana nilikuwa hata sina mwaya, basi tu nafanya revenge!
Mtoto wa mama mkwe ambae ni mume wangu akanigaaanda nikatuliza akili nikasema lazima nijue chanzo kwanini baba yangu alikufaaa nikasema namtumia huyu son of a beyaaach mpaka kieleweke
Tukaanza mahusiano, mwezi wa 1 mw
ezi wa 2, mwezi wa 3 me nafekisha tu mapenz jamaa kakolea
Tukamaliza mwaka, akaona isiwe shida tuoane nikaolewaaa me kusema ukweli wala sikumpenda nikaolewa mama akiwa na wasiwasi nimeolewa nimekaza rohoooo simpendiii ingawa watu wanamwita handsome, oh you so lucky, jamaaan mume mzuuuri me hata siuoni huo u handsome nipo kwenye mishen tu hapa
Nikaanza kuishi maisha ya high class, 1st class kila kitu, 1st class food, flights, hotels, high end cars naendesha kama Evoque, Ford Rangers, Audi ndio gari zangu hapa hapa Tz wala sio ulaya lakini hayo hayakunirubuni maana nilikuwa kwenye mishen
Nikaanza kufukua mafaili yaliolala kuangalia babangu alikuwa anafanyaje kazi, nikampata mzee mmoja alikuwa anafanya hapo kama mlinzii akatimuliwaaa baada ya babangu kufaaa
Nikamtafutaaa nikaja kumdakaaa alikuwa mikocheni shoppers plaza tena tuligongana kikumbo nikamwomba msamaha, aliponitajia jina nikajua ndo mwenyewe nikamtoa lunch nampa hela kuomba msamaha nimemgonga kipepsi
Baadae yule mzee akauliza we mwana mbona kama nakufananisha na mtu m1 akamtaja baba yangu nikamwambia me mwanae pekee akafuraaahi sana, tukawa mtu na mwanae sasa
akanikaribisha nyumbani kwake uswazi huko temeke alikuwa anaitwa Mzee Guibuu!
Nikafika mtoto wa Oysterbay naenda Temeke ndani ndani unakaribishwa kwenye mkekaaa, nikakaa mwenzangu mbele ya kifo cha babangu ntakaa hata kwenye mavi
Wenyewe wanaona aibu kunikaribisha kwao mtoto wa kishua!
Nikamwelezea shida yangu yule baba alilia sanaaa sanaaa sanaaa akaniambia mwanangu mimi nipo hapa
Sababu ya huyo babako marehem nipo nje kwa dhamana nilitakiwa nikae jela
Tukaongeaaa kucheki saa saa 1 usiku njia ya kurufmdi sijui nimepaki audi nje watoto wa uswazi wamejaa wanashika shika wanashangaaa leo kwa babu Guiduu kuna nini?
Tukapanga mikakati ya kusaidiana nikamwambia mzee nipo radhi nikubadilishie maisha sina amani babangu amekufa kifo cha mende najua yule mama amemuua
Mzee Guibu:
akazidi kulia mwanangu embu acha by gone iwe by gones
Gigi:
haitakaa iwezekane lazima nijue hapa nina hasira nina pain lazima nijuee
Mzee Guibu:
sawa mwanangu sasa tufanyaje
Gigi:
nakuhamisha hapa kwanza uishi sinza pili nataka unitajie kiiila kitu cha hapo ofisni mambo yalivyokuwa yanaenda mpaka akafa
Cha tatu ukitaka urudi kijijini nikununulie eneo sawa tu ila kesi yako ya mahakama me nalipia kila kitu kwa dhamana!
Mzee guibu akafurahi sana akasema sawa mama nitakusaidia akanieleza kiila kitu kuhusu mambo yalivyoenda akanipa na majina ya wafanyakazi waliokuwa pale walioondolewa ambao walijua kwanini baba yangu alikufa nikaondoka kwa yule mzee saa 7 usiku nikachukua namba yake ya simu na mkewe akanisindikiza mpaka barabara kuu nikaondoka
ITAENDELEA

0 Comments:
Post a Comment