ON MY HIGH HORSES PART 5



Chombezo : On My High Horses
Sehemu Ya Tano (5)



Aaliyah: maskini pole sana jamaaan

Gigi: embu njoo hospital basi tuongee

Aaliyah: nipo best rest remember?! Siwezi nitakuja na mume wangu

Gigi: we Aaliyah kumbe ndo ulivyo ee, hauna hata shukrani no wonder Mark alikuacha

Aaliyah: ndio maana na wewe ulimwuua mumeo stupeeeed kaa na mlemavu wako mwenyewe shenzy, simu ikakatwa!

Gigi ana hasira hana hata hali, akampandia hewani Mark

We mark, hunijui sikujui lakini nimekuta namba yako kwa Best friend amelazwa amepooza kuna pesa za matibabu zinahitajika maana sijaona kadi yake ya bima ya afya

Mark: uuuwi jaman Best Friend wangu,  naja naja naja mamaa najaaa

Baada ya dk 20 Mark akadondokaaa akaenda kuskiliza nini kimetokea akaelezwa cha uongo

Oh kuna demu alikuwa anampenda kusikia kaolewa akapaniki akaanza kupumua hawezi ndio kuzimia kuja kushtuka dokta ananiambia amepooza sa sijui ndugu zake wala nini

Mark akampandia hewani mzee na Maza yake wakaja pale maza yake na Best friend analia kweli kweli baba mtu haelewi akaelezwa akauliza Gigi amtaje huyo demu

Gigi: hayupo tz anaishi Urusi na huyo bwanake harudi leo wala kesho ( kha! Gigi kwa uongo ni noma)

Baba wa best friend akachoka basi wakaendelea kuuguza

Gigi akampandia hewani Tausi we hawara ya Best friend, bwanako huku amepooza njoo okota mzoga wako akamtajia na room namba

Baada ya lisaa 1 Tausi akadondoka na dera kama kweli kumbe mshenz tu
Akajidai pale analia lia, Gigi anamwangalia tu shubabti mkubwa anamzoom tu na drama zake

Baadae akamfuata akawa anaongea na Tausi

Tausi: jaman imekuwaje wewe ni nani

Gigi: mimi dadake, cousin ya best friend, mamake na Best friend ni shangazi yangu, Tausi akakubali

Gigi akaelezea ule ule uongo wake hakosei Tausi akaamini

Basi Tausi akamsahau bwana wake, kila siku ndo kushinda pale na nene

Gigi akajitoa likizo kwa mwezi anakuja mara 4 tena j2 tu si unajua tena cousin sio kila siku lakini Tausi hapo kiiila siku yupo na mama Best friend

Baada ya miezi 3 Best friend akafungua macho, dokta akajaribu atembee akashindwa

Akalazwa tena mwezi wa 4, anapelekwa mazoezi, anarudishwa, mwezi wa 5... mwezi wa 6 .. mwezi wa 7... mwezi wa 8 uzuri Bima ya Afya inalipa!

Baada ya miezi 9 Aaliyah akawa anajiandaa kujifungua na wala hajawahi kwenda kumwona Best friend kabisaaa

Mwezi huo wa tisa na wiki 3 akajifungua watoto mapacha, wakike na kiume

Baba Bonge akafurahi sana, kha! Akawaita majina ya marehemu wazazi wake baba bonge, 9 kumi watoto alijifungulia pale pale alipolazwa Mark, wazazi wa Mark wakaenda kusabahi wajukuu,

Baadae Aaliyah akaomba uzazi akalelewe kwa wazazi wake sio kwa mumewe na Baba Bonge kijijini akakubali
Baada ya siku 4 wakatoka hospital maana Aaliyah alijifungua kawaidaa

Gigi akasikia kuwa Aaliyah amejifungua watoto mapacha hapa hapa hospital maana alikutana na wazazi wa Aaliyah wanapeleka msosi kwa aaliyah

Gigi: jamaaani mimi sijui chochote wala sijaambiwa kitu mbonaaa!



Gigi a
kampandia hewani aaliyah akiwa kwenye gari yake akakuta namba unayopiga haipoo

Gigi: mxiiiiuuu, akamfuata nyumbani kwa mumewe baba bonge akaambiwa haishi hapa tena wamehama nyumba, akauliza wapi mlinzi akamwabia sijui mimi

Gigi akaenda mpaka kwa mama Aaliyah akashangaa anakatazwa kuingia na mlinzi akajua tu ni Aaliyah na mahasira yake akaondoka kwenda kumtafuta Babu mlinzi akamkuta hayupo bado hajarudi bondeni dah akaona arudi tu kwake akapange tena mbinu mpya maana wapiganaji wake washafeli

Mama Bonge:
Naskia babako amepata watoto mapacha na huyo hawara yake aliemuoa

Bonge: eeeh! Makubwaaa mimi hata sijui! kazaa na nani

Mama bonge: kuna malaya mmoja anaitwa Aaliyah!

Bonge akachokaaaa! Mama unasemajeee?! Huku ananyonyesha mwanae Mark the 2nd

Mama bonge: nimekwambia anaitwa Aaliyah, vepee unamjua au?!

Bonge: namjua?!kwani mama wewe ushamsahau Aaliyah?!

Alikuwa bibi wa Mark ukawatenganisha

Mama Bonge: heeee?! unajua nimemuona mara 1 t
uu doh!
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Bonge: kweli Malipo ni hapa hapa Duniani! Mama Karma imekurudiaaaa?! uuuwi huku anacheka

Mama Bonge: sasa unacheka nini na wewe buana?!

Bonge: aaaah, pole mamangu, ahahahahaha yule ambae ulimwibia mume amekuibia wako?!

Makuuubwa kweli Mungu yupo, inakupasa ukatubu dhambi zako zote mapema maana huko mbele pabayaaa, tena baba baada ya kuwa na wajukuu anakuwa na watoto, uuuwiiii haya bwana bibi wa mapacha umekuwa

Mama Bonge: embu niache mimi, kwa sasa nipo single hata na mimi nikitaka kuzaa nitazaa vile vile!

Bonge: akawa anacheka tu huku anamnywesha mwanae maziwa kwa chuchu za chupaaa

Mama bonge akaondoka, akaenda kukaa chumbani kwake, mara simu ikaitaaa kupokea kumbe ni lawyer

Lawyer: mama za masiku

Mama bonge: salama baba

Lawyer: nilipata mzigo wako mama sasa nakukumbushia ile kesi mama ni mwezi ujao uwe tayar kupanda kizimbani na watu wako uwaandae

Pia itabidi wiki ujayo tuonane ili tuwekane sawa jinsi ya kujibu maswali ya mahakama na watu wako pia wanatakiwa waje niwapange wale mashahidi wako

Mama Bonge: sawa babangu asante sana kunikumbushaa simu ikakatwa

Mama bonge akaumizwa kichwa weeee, haelewi itakuwaje hana ushahidi wa kutosha kumweka Gigi mahala pake pa aibu na kwenye matesooo na kumshinda kesi alioifungua, maana mume ndo huyo kaondoka na kimada umri wa mwanae wa mwisho dah sasa nafanyaje maana hata huyu hawara wangu hana ushahidi wa kutosha

Akawa anawaza na kuwazua akaishia kulalaa

Asubuhi kukakucha Gigi akapigiwa simu na Lawyer wake

Lawyer: mama salama?!

Gigi: salama

Lawyer: sijakuskia

Muda mwanangu vepee! Unajua kuwa kesi yako yaanza kuskilizwa wiki ijayo?!

Kuna pesa za kunilipa natakiwa nionane na wewe ili tuweke sawa jinsi utakavyotoa ushahidi pia huu ushahidi wako una nguvu ila nahitaji kuona watetezi wako?!

Hii ndo kesi ya mwisho tupate hukumuu jitahidi uje unione wiki ijayo sawa?!

Gigi: dah baba asante sana kwa kunikumbushaaa! Nilishasahau asante sana, sawa naja wiki ijayo simu ikakatwaa

Dah afadhali kesi ianze maana nishaona Dunia chungu sasa, nani atanisaidia kesi maana sasa huyu babu mzee keshaingiwa na hurumaaa

Akampandia hewani babu mzee hapatikani dah hii ni noma, akaenda nyumbani kwake akamkuta hajarudi ulizia mlinzi akamwambia atarudi wiki ijayo

Ulizia namba ya simu ya bondeni akapewa akampandia hewani baba baba baba rudi tz haraka kesi mwezi ujao lazima tujipangee mimi huku mambo yameharibika kabisaaa hamna msaada nakutegemea wewe tu hapa tafadhali usiniangushee

Babu Mzee: sawa mwanangu nitakuja kabla ya kesi maana huku nishapata kimwana napeleka mahari wiki ijayo naoaaaa kwaiyo nivumilie nitarudi kabla ya kesi

Gigi akachokaaa anajutaaa kwanini alimwambia akaoeee akamjibu kwa unyonge sawa baba hamna neno.

Gigi akatafakariii anaona ushahidi hana na hivi Best Friend kawa zoba na Aaliyah kajifungua akajiona yupo pekeyake akachoka akarudi home kulala

Mchana huo mama bonge akaonekana Kanisani kwa akina Gigi, akaingia ndani ana appointment na Mama mchungaji

Kuingia ndani wakasalimiana hapo wee, wakakumbushiana kumbe ni ma best wa siku nyingii

Mama Bonge: sasa mami
Wangu nina kesi mahakamani nakuhitaji wewe na mumeo mnisaidie kunitetea

Kuna katoto kalikuwa kakwe changu lakn ndo ivyooo tenaaa, alipeleka kesi Mahakamani kunishitaki mimi nifungwee lakini sasa sina ushahidi tosha, akamwagia ubuyu weee

Mama Mchungaji: akachekaaaa wewe mama bonge acha basi kunitania, huyu Gigi unaemsema wewe ni Gigi wa hapa kanisani kwangu au?!

Mama Bonge: Gigi anasali kwako?! Makubwaa una picha nimwone?!

Mama mchungaji: sina ila kama una picha yake we nipe nitakwambia kama ndie au sio

Mama Bonge: akatoa picha ya mkwewe Gigi

Mama mchungaji: ah ndio huyu mkweo?!

Basi anasali hapa lkn mbona ni mke wa mtu, mume wake anaitwa Best friend wana hela sana wanatoa sana wanajitoa Kanisani, mume wake si mwanasheria

Mama bonge: heee! Gigi kaolewa?!

Iyo mpya na nani?!

Best friend?! Hili jina mbona kama sio geni kwangu!?

Embu ngoja akampigia mwanae Bonge eti unamjua mtu yeyote anaitwa best friend?

Bonge: si best yake na mume wangu Mark?!

Mama bonge: ah sawa nimemkumbuka, ivi huyu best friend alioa?!

Bonge: mmmh sijui ila sidhani mama, sijaskia hata kwa Mark ila nimeskia ameparalyse juzi kati hapa Mark alienda kumcheki hospital na kwao maana alisharuhusiwa siku si nyingi sasa sijui kama ameoa ngoja namwuliza Mark nakujibu, simu ikakatwa

Mama mchungaji: vepee tenaa kuna shida?!

Mama bonge: nimeshamjua huyo mume unaemwongelea basi kama wanasali hapa ni vizuri, ila huyo mumewe best friend naambiwa ame paralyse yupo kwa wazazi wake kwani hamjui

Mama mchungaji: hapana wewe ndo unaniambia wala sijaskia
Kabisa

Mama bonge: ndo ivyo mama ndo ivyoo! Sasa turudi kwangu... kwasababu unamjua huyu Gigi itakuwa poa sana kama utatoa ushahidi Mahakamani kuhusu yeye

Kuna kimeo nataka unisaidie kutoa ushahidi kuwa Gigi ni pretender hajaokoka na unamfahamu vizuri sana

Mama mchungaji: mama bonge hapana iyo ni dhambi kwa Mungu Muumba siwezi fanya ivyo

Mama bonge: tena utamwambia amekuja kuficha makucha yake kwasababu kuna kesi anayo mahakamani ni mtu mbaya na amekiri kwako kuwa amemuua mwanangu yule aliefariki

Mama mchungaji: hapana mama bonge hio mipaka mibaya sasa tunavukaaa

Mama Bonge: utaiambia hivyo iyo Mahakama la sivyo nakushitaki na utanilipa pesa zangu nyingi tu

Mama mchungaji: siwezi fanya ivyo na wala usinitishie maisha

Mama Bonge: wewe mama nadhani haunijui kabisa, mimi ni israel ninaetembea sijafaaaa, utanilipa fedha zangu zoooote nikikupeleka Mahakamani wewe kwa matendo mabaya yote ulionifanyia hili kanisa utalifunga shenzy kabisa, akaingiza mkono kwenye pocho yake akatoa picha za mama mchungaji amelala na mumewe (baba bonge) akamchana live nitakufunga na utanilipia fidia wewe ndio umesababisha mimi na mume wangu tumeacha,

Pia picha hizi za mumeo ametembea na kila mtu mpaka Gigi unaemwona malaika

Mama mchungaji akatoa machooo, kweli mama Bonge Mafiaaa mpaka picha za Gigi na mumewangu anazo, najua nilikuwa nahisi lakini hii ni tooo muuuch

Mama Bonge akatoa picha za mama mchungai na Best friend wakati wanapeana raha hapo Kanisani, hotelini, Mama Mchungaji akachokaaaaa! http://pseudepigraphas.blogspot.com/

Kweli nimemkubali mama Bonge Mafiaa


Mama Bonge: akatoa picha za mama Mchungaji na wanaume aliolala nao mtaani, aliolala nao pale kanisaaa wazee wa kanisaaa kha!

Aibuuu



Nikizipeleka hizi mahakamani kanisa lafungwaaaa sasa unasemaje?

Utatoa ushahidi kinyume na matendo ya Gigi au?!

Ni bora kumkosa mtu mmoja ili uokoe maelfu ya kanisa lako, hata mafarisayo walimtoa Yesu kuokoa kanisa zima

Mama mchungaji: kwaiyo mama bonge unajua Neno sasa sio?

Mama Bonge: usipofanya kama navyokwambia nitakuweka pabaya nimeshakwambia, mimi ni israel ninaetembea utaniona mwanga na mchungu Tz utahama kama hautalala hela na mumeo namchukua mimi

Mama mchungaji: mchukua hata sasa ndio maana umeachwa na mumeo shenz kabisa

Mama bonge: mimi sina cha ku loose, nina wajukuu 4, nina pesa na mali kibao, wewe una nini?!



Watoto wako wapo wanasomaaa tukifunga kanisa hao watoto wanakuwa machokoraaa hawataenda shule, tena nitakuweka pabaya, endelea kunitukana

Sasa kama nilivyokwambia, j5 wiki ijayo address hii ni ya lawyer wangu na simu yake nenda kamwone, tafuta evidence zooote za Gigi mbaya na nzuri mpelekee atakuelezea jinsi ya kufanya na kuongea Mahakamani
La sivyo huu mwezi utauona mchunguuu

Mama Bonge akaondoka akabamiza mlango

Mama mchungaji akabakia mdomo wazi ameduwaa hajui anafanyaje




Aaliyah buana mtu wa surprise, akamwibukia Best friend kwaooo, akawakuta wazazi wake akaongea nao fastaa akamwona mgonjwa

Best friend kumwona Aaliyah analia tuuu! Machozi yanamtokaa

Aaliyah: best friend jaman pole, nisamehe i did what i had to do nimekufumania sasa na Gigi you leave me no choice, wazazi wa Best friend walitoka nje hawakuelewa ni nini

Aaliyah akaongea weee akaongeaaa akaongeaaa Best friend anatoa machozi,

Aaliyah akamkumbatia amamchumu mashavuni akamchumu mdomoni, good bye Best friend get well soon akaondoka

Best friend: akatoa machozi pale wazazi wakaja wakampeti peti usijali Mungu yupo atakusaidia utapata mwengine,

Best friend akanyamaza akatulia kabisa, baada ya siku 3 Gigi anapigiwa simu mama Best friend analia, Best friend Amefariki

Gigi hakuelewa akadondoka kwa mamake Best friend maiti ipo mochwarii alilia Gigi jaman kama mtoto mdogo utadhani amemzaa best friend

Akamwuliza mama nini tena mbaya akaambiwa 3 days ago alikuja Aaliyah akaongea nae akawa anatoa machozi, baadae akaonekana kuchangamka lakini baada ya siku 3 akafa usingizini kapelekwa hospital dokta anasema ilikuwa stroke amewaza sana tukajua labda aaliyah kamweleza kibaya kumbe walaa ni maneno ya kawaida yule binti alimweleza kwanini aliolewa na huyo alieolewa nae, maana tuliskiliza maongezi kwa cctv camera yetu hakuna baya alilomwambia wala kumpa

Gigi akachokaaaa: akampandia hewani Aaliyah hapatikani, akaona ngoja wamalize msiba kwanza
Msiba ukakaa siku 3 watu kibaooo wakaja akina Mark akina Tausi wanalia hawaami i maskini Best friend kama utaniiii, hadi

Mama mchungaji wa kanisani nae kajaaaaa chezeiya fake lawyer, badae wakazika makaburi ya kinondoni, watu wakaondoka lakini Gigi hakuondoka, akabakia kwenye kaburi analia tu analia tu haelewi imekuwaje Best friend jamaaan umeondoka umetuacha na wazazi wako tunakutegemeaa kwanini lakini Best friend kwanini katukana weee alipomaliza hasira yake akaondoka kurudi nyumbani kwake Best friend hayuuuupoooooo teeeeenaaaa, SHOW IKAISHAAAAA

I Vacationed in Hell

Baada ya msiba na wiki ikapita maana Gigi aliomba udhuru kwa lawyer wake, akapata simu kwa Mama mchungaji asijue hili wala lile akaambiwa aende kanisani,


Gigi: mImi bado nipo kwenye wiki na msiba mume wangu hata 40 sijamaliza siwezi kabisa nipo kwa wazazi

Mama mchungaji: mama mimi sio type ya kuchezwa huyo marehemu sio bwanako wala nini, mmekuja kanisani kwangu kunizunguka na Mungu kawalaani ndio maana kamwondoa shenzi kabisa

Gigi: akabonyeza record kwenye simu yake, mama kwani tatizo nini tena mbona wanizidishia machungu jamaaa?

Mama mchungaji: unajua wajinga na washenzi kama wewe huwa siwapendi kabisa ukitaka uwe salama hapa Tz ujisalimishe kwa pilato mwenyewe

Gigi: mama nadhani haujanielewa mimi siji nipo kwenye 40 ya mume wangu mpaka miezi 2 ipite nitakuja kukuona otherwise njoo wewe si unapajua nyumbani?!
Njoo, kuja kuniona ni moja ya huduma pia

Mama mchungaji: akakata simu

Gigi: akawa anawaza kuna nini mbona maza leo kageuka mbogo?! Nikienda nita prove kuwa ni dhaifu nikikaa nitaonyesha uimara wangu na umakini lkn mama kuna maneno kaongea sijaelewa embu ngoja niwashe antena alizowekaga marehemu best friend

Kuja kufungua mama mamaa mama mama kumbe mama bonge alishaenda kumlisha tango pori, kamtishia mineno akawa anairekodi ile convo yoteeee, akashtuka na hivi best friend hayupo akaona vita anaicheza mwenyewee kesi yenyewe hii imebakia wiki 3 tuingie Mahakaman sasa afanyaje

Akamcheki babu mzee bado anakula raha akamtonya best kafariki babu mzee hajashtuka mimi nipo na mke wangu
Kurudi tena tz sahau huyu kimwana amenichanganya sana sana sana

Gigi: akaona isiwe shida huyu baba naona kaamua kunitelekeza

Basi nipe zile evidence basi za Vera mama bonge

Babu Mzee: haloo haloo halooo sikuskii unakatika haloooo simu ikakatwa

Gigi: huyu ananiletea michezo ya kizamani hajui mimi mwenyewe wa zamani ngoja nikamfanyie umafia kwake ataisoma namba

Jioni saa 12 nanusu akatia timu kama jambazi nyumbani kwa Babu Mzee mlinzi akawa amekaa akasubiri asinzie sinzie akaondoka, ikafika saa 3 akarudi kumkuta amejilaza kwenye kiti chake akamchoma sindano kwa nguvu paaa akaingiza maji akachomoa fasta,

Mlinzi kushituka anasikia kitu kimemchoma sana lkn hakionii, akasimama kuangalia mazingira shwaaari akarudi kukaa akajikunyata hapo inaenda 4 usiku mlinzi akazama usingizini

Gigi akaingia kama komando yoso akafunga gate vzuri sana

akaingia home kwa Babu mzee akaziua ua cctv camera toa kila kitu zima kila kitu, mpaka anamaliza ilo zoezi hapo saa 6 usiku

Akaingia bedroom yake akaanza pekua pekua na wewe pekua pekua kila kitu akakutana na ile cd aliokuwa anam blackmail mama bonge mpaka akakubali kutoa talaka, pekua kila kitu kipo safi on mama bonge's favor, pekua pekua nyumba nzima hajapata kitu akamind, saa 9 usiku akasema ngoja nilale kidogo, akashtuka saa 11 azana ya waislam akaondoka amemwacha mlinzi kazimaaa anauchapa kiroho mbaya sio kitoto

Akawa amekaa anatunga tu sheria akaona hii kesi akishindwa hatopata uhuru wake akaondoka akaenda zake mpaka kwa lawyer, akaskiliza kwanza lawyer vepe?

Lawyer akamwambia mama tupo pabaya kusanya taarifa zako zooote za ukweli haraka kesi imekaribiaaa

Gigi akaondoka kwa lawyer amechokaaa hapo kejambishwa jambishwa kuwa atashindwa kesi akarudi nyumbani kutafakari akakumbuka chalii yake aliomba kumsaidia mpaka mauti akajivisha kama bibi wa kizenji akadondoka zenji full mass nondo pemba moja

Akatua kwenye koroboi baya baya, akaingia katembea akatokea mpaka baharini, kha kweli Gigi kaamua maana kuna ka mwendo toka koroboini mpaka kwa huyo best yake.

Ni umbali kama toka Mwenge mpaka Morocco, ilo ni zoezi tosha..

Kufika anamkuta rafkiake amekaa anapunga upepo kifua wazi.

Akamwita Marioon

Marion: kageuka, Mungu waaangu Gigi my love umekuja?

Wakakumbatiana my Gigi umepotea sana

Gigi: nimefika rafiki

Marion: unaendeleaje, unaonekana mpweke sana vepee!?

Gigi: not good Marion hali mbaya sana na sijui kama nitaondoka nchini

Marion: nilikwambia my love, yule mama mafia, nilikwambia usishindane na mama wa kimachame atakuua, usinge feli kesi yako ungechukua hela alizotaka kukupa!

Gigi: lakini mauti ya Babangu inaniuma, sikuweza kuondoka kiboya boya kama mtu alieshindwa!, noo

Marion: basi nambie nini wataka

Gigi: kushinda kesi na kuondoka nchini vizuri, nataka nikakae Marekani nisirudi tenaaa

Marion: plan yako ipoje

Gigi: akamwelezea wee wakaingia kazini,

WAKATI HUO HUO...http://pseudepigraphas.blogspot.com/

Mama bonge akampandia hewani mamchungaji, mbona haujaja kwa lawyer

Mamchungaj: akakata simu

Mama bonge: ah hanijui ee, ngoja nimwonyeshe show zangu

Ikafika j2, mama mchungaj na mumewe wanajiandaa kutoka kuwahi ibada ya kwanza, dereva hayupo, simu hapatikani, wakaondoka kwenye gar kuwasha haiwaki, wakaenda kwenye gar ingine ikawaka, matairi 2 flat tire, dah kuangalia saa saa 1 kasoro 5 asbh, kumpigia simu mchgj msaidiz hapatikan, basi wakaona watembee mpaka kwenye taxi dk 20 wakapata kufika church saa 2 kamili asbh kuingia ndan wanamkuta dereva anasifu anaabudu wanashangaa, mchgj msaidiz nae buzy anaongoza ibada watu wanaomba

Ibada ikaisha wakamwita dereva vepe mbona haujatufuata

Dereva: nilipata sms ya mama mchungaji kuwa nisije mtakuja wenyewe, akawaonyesha.

Mamchungaj anashangaa mimi sijatuma jamaa, mumewe na dereva wanamshangaa, huyu vepe mzima kweli?

Mamchungaji anakomaa sijatuma sijatuma.

Wakamwacha, wakarudi nyumbani saa 10 jioni mlinzi hayupo alafu nyumba inawaka moto upande m1

Wakaita majirani wakabomoa geti bomoa mlango wakamwagia mchanga, maji mpaka wakaumaliza.. Wanashangaa tuu shetwain wa j2 vepee?

Wakalala ivo ivo, asbh wanapigiwa simu kanisa laungua mama,

tunazima hapa unashindikanika, mamchungaj kahaha anamwambia mumewe waende hawana gar iwakapigia taxi hapatikani, wanapiga kwa mtoa taarifa hapatikani, wakachukua taxi mpaka church kufika hamna cha moto wala nini, wakamwuliza muhusika aliepiga simu hamna hajapiga simu yangu ilikufa nina mwezi wa 3 sina simu, mamchungaj akaanza kushangaa, mumewe anamwuliza vepe mama unakuwa mgonjwa skuizi au?

Mamchungj anashangaa mimi sio mgonjwa nimesema kweli jamani, wakaamua wampumzishe nyumbani

Akalala siku ya 1 ya 2 mumewe anamfuata mke wangu kuna kesi inakuja tuisikize, wakaja waleta kesi mama m1 anamshtaki mama mchgj ametembea na mumewe akatoa picha zile zile alizoonyesha mama bonge.

Bamchungaji anashangaa mkewangu aibu gani mama mlalamikaji analia anatukana mimi nateseka kwa mumewangu we unakula raha nyama wee, mimi naondoka ila Mungu atalipa akaondoka.

Mamchungaji akamkumbuka mama bonge akajikausha, siku akawa anaenda sokoni na dereva kufika sokoni ananunua vitu akaja kichaa na fimbo akampiga kichwani mgongoni began usoni mama analia watu hawamsaidii wanamwangalia tu, bdae dereva anaona mbona makelele akafunga gari akaenda kumcheka bimkubwa anavuja damu kambeba hospital moja akalazwa.

 Mumewe akaja kumsabahi akamwuliza hajibu, akaondoka, usiku saa 6 akaingia mama bonge, akawa anamshangaa ameingiaje, akamsalimia pale

Mama mchungaj: unafanya nini hapa? Nani kakuingiza muda huu?

Mama bonge: umenisoma sasa ee? Ndio ushanielewa au bado?

Mama mchungaj: mwuaji mkubwa

Mama bonge: hata sasa naweza chomoa mipira ukafa, usicheze na mimi

Mama mchungaj: jaribu uone nabonyeza emmergency

Mama bonge: bonyeza tuone kama inafanya kazi,

Mamchungaj akabonyeza pale hamna kitu

Mabonge: sasa nakuua hapa hapa, amua utanisaidia au la?

Mamchungaj: akanyamaza

Mabonge: amua, akatoa mkasi, nikate mpira niache?

Mamchungaji: go to hell

Mama bonge: i vacationed in there

Akakata mpira wa mamchungaj wa upumuaji , mamchungaj akawa anahaha kupumua

Mama bonge: i'll see u in hell moron,

Akamfunika na mto akawa anahangaika kupumua mpaka akakata roho, mama bonge akaondoka amemwacha mama mchungaji hayupo tenaaa


Asbh bamchungaj akapigiwa simu kuwa mamchungaj hatunae, amefariki usiku, alichomoa waya wa upumuaji maana tumecheki cctv zote hamna mtu alieingia ndani kumdhuru kabisaaa,

Poleni sana baba mchungaji sisi tumechunguza tumeona kuwa mkeo
amejiua kwa kudhamiria

Dah bamchungaj akalia wee kama mtoto mdogo, wakaja wazee wa Kanisa baada ya masaa 2 kumsabahi.

Siku ya mazishi mama bonge akaendaa, kama stranger makaburini kakaa mbaliii, anazoom na mpenz wake mpyaa wa miaka mingi

Msoma taarifa za marehemu anasoma: marehemu alianza ku behave ajabu ajabu these last few days, mara atuambie kanisa limeungua mara anatumia watu sms kuwa wasije kutuchukua mara katembea na mume wa mtu mke kaja kulalamika ila ktk uchunguzi tulidhan yule mana amemdhuru ila imeonekana yule mama tangu atoke pale nyumbani alirudi kijijini kuuguza mamake!

Akaenda sokoni akaanza kupigwa na kichaa hatukuelewa kuna nini, akafikishwa hospital kwa mahututi ya kupigwa ndipo hapo mama mchungaj akajiua akiwa hospital ICU

Watu msibani wanaangaliana, hawaelewi hili movie vepee?!



http://pseudepigraphas.blogspot.com/

TUONANE TAR 27 APRIL 2018 SAA 1 USIKU YA TANZANIA.

________________________________
D. The good, the bad and the evil


Msiba ukaisha mchgj akawa anaomboleza na nini, wakaja wamama, wajane, wamama senior bachelor, wadada toxic bachelor, wadada single, basi kila mtu na pole yake ushuzii





wale wamama wa mjini waliotembea na Mchungaji

wadada walioahidiwa ndoa,


yani ni balaa,




izo kumbatio sasa doh,



Ninauhakika Marehemu alikuwa anazunguka kwenye kaburi huko alipo akiona haya majanga! sio kwa ufuska ule,



Watoto wa marehemu wanashangaa mama kaondoka ametuachia matatizo, Maana shoo ya kutoa pole utadhani maonyesho ya ulimbwende,



Mavazi sasa na flirting ya kufa mtu, vimini, leggings, basi kila siku hakosi mwanamke amekuja kutoa pole kwa Mchungaji Mgane



Wengine kupika, kufua, kudeki na Pastor mwenyewe alivyo mzinzi kila mtu anamnong'oneza kivyake,



wewe unafaa kuwa mke, mara wewe utanifaa, mara mkewangu wife nakuona, basi kila mwanamke anavimba kichwa kivyake, jitihada za kufua mwenye hela walipeleka kwa dry cleaners, mara menu ya hotels inayoletwa ni hatari,
watoto wa marehemu wanaishi paradiso ndogo hahahaha



Basi pastor akapata mwaliko kwa mama m1 senior bachelor akamfanyie maombi nyumbani kwake kumbe anategwa!



Mgane Pastor asijue mitego ya ibilisi maana ye mwenyewe anakula na ibilisi sahani moja,



Akaenda, kufika maza akamwita chumbani, huku ndio napata mashambulizi Pastor akaenda kutoa huduna ya kiroho kaanza kuombea pale akiwa ktk kumaliza yule mama akatokeza uchi wa mnyama, Jesus! mgane Pastor anashangaa,



Mgane Pastor: jaman we mama mimi sipo ivo nafanya shughuli ya bwana



Senior Bachelor: usijali Pastor hata hii nayokupa ni huduma tosha,



Ni shukran ya pekee kwako,



Umenifukuzia mapepo ila ukanisahau kuniombea na mimi sasa unaonaje ukaja kunibatiza kimwili ili niishi vizuri unajua sijawahi kupata mguso wa mwanaume kwa miaka 20 sasa tangu niokoke na maisha yamekuwa magumu sana kwangu na ya shida



Mgane Pastor: akajibwida akambeba senior Bachelor wa watu, wakazama Honey Moon,



Pastor nae havumi lakini yumo jamaaan, mechi anaiweza






Senior Bachelor hakutaka usiku uishee alitaman mechi iendelee lakini ndo ivyo akawa anakazana kuwa kwenye ule wakati (live into that moment)



Huko Pemba:



Gigi akaonekana yupo na Marion wanapanga makuu,



Mesenja wa Marion akamletea ripot Marion akatikisa kichwaaa... akamwambia Gigi, mimi nilikwambia kuwa huyu mama ni muuaji kabisa

Angalia amemuua Mama Mchungaj wa pale kanisani kwako, angalia hizi picha za msiba walikuwa wanazika makaburini, angalia za kuaga



Gigi: MUNGU WAAANGUU, sasa tunafanyaje

Wiki zenyewe zimebakia 2 tu mimi mbona nachoka zaidi jamaa sasa tunafanyaje?!



Marion: lazima tumjambishe jambishe lazima nitume vijana wangu wakafanya kazi ya kumchunguza tujue nani yupo juu yake tumpindue



Asbh kukakucha vijana wa Marion wakaingia Dar es salaam, wakapiga usnitch wanamzoom Mama Bonge anajiachiia kweli kweli mpaka anaenda kwa uyo bwana ake wa miaka mingi



Wakamzoom Bonge wakajua anaonana na matusi

Wakapeleka ripot ndani ya siku 2 badala ya 3, wakaambiwa warudi kwa Mchungaji, kwenda kumcheki Mchungaji anahama nyumba hadi nyumba



Gigi akamwambia Marion kuwa ana mzee wake m1 hamsomi somi anahisi anampendelea Mama Bonge na mimi nipo pekeyangu yupo huko bondeni



Marion: kwaiyo unataka tumfanyaje sasa huyu Mzee



Gigi: mpige jamba jamba mpaka aje aungane na mimi staki ujinga ajue mimi ndio Gigi the great na atoe ushirikiano mpaka nishinde kesi




Marion akatuma vijana wake 3 bondeni Africa Kusini kwenda kumrejesha Babu mzee wakatua bondeni, kumsaka babu mzee mwenyewe anakula kula raha hamna cha mke wala nini?



Wakampa jamba jamba wakakamata mishangigi ya kizulu ikamfilisi wakamwibia passport babu mzee wakamwitia na polisi akarudishwa Dar hana hata hela kufika Airport ana buku akapanda daladala mpaka kwake Bunju hakufunguliwa na mlinzi kuangalia nyumba shaghala baghala,



Hamna cha msosi, simu hana dah alichoka sana




Akakaa siku 3 njaa kali akaenda dukani kwa Mangi anaomba simu akampigia angalau Gigi, Mangi akampaa!



Babu Mzee: Mama salama nimesharudi Dar vp waendeleaje



Gigi: vibaya sana nipo tu sina hata 100

http://pseudepigraphas.blogspot.com/

Na ile kesi ni wiki 2 zijazooo basi nimeona nishindwe tu



Babu mzee: hapana Gigi usikate tamaa nitakusaidia



Gigi: kivipi? alafu mimi sina hela hela zote nimepeleka kwa lawyer sina hata 100



Babu Mzee: basi mama uje tuyajenge hamna lililoharibika, njoo tafadhali



Gigi: kama unataka kunisaidia nenda kamwone lawyer wangu kesho mpe vithibiti (evidence) vyako vyote, vinginevyo potezea akamtumia amwani na sehemu anafanya kazi lawyer,



Babu Mzee hapo kachoka hela kabakiwa na 200, akaona auze kitu kwa jirani akapata elfu 20, akaenda kumwona lawyer akampa evidence akaondoka, lawyer akampigia Gigi akamweleza Gigi akacheka akamwacha Babu Mzee ashike adabu kidogo hapo kwake



Huko Pemba Gigi akawa mwenyeji, anazurura wee anawafanyia wazungu utalii mara alale na wazungu, basi balaa tupu,



Marion akampigia simu wewe kimwana upo wapi?! Gigi akamwelezea



Marion: njoo hapa nyumbani kuna dharura ya balaa



Gigi akakimbia kufika anaambiwa fungua hii sahani kufungua tobaa kichwa cha matusi



Anamwuliza Marion huyu nani?!



Marion: vijana wangu wamekuletea kichwa cha Matusi,



Hayupo tena, bado tunamsaka bwana wa Mama Bonge wa miaka Mingi



Matusi alikuwa Bwana wa Bonge ndio aliempa ujauzito wa Bonge, na team yake yote wameisha bado tunamalizia team ya mpenzi wa mama bonge, mpaka sasa 50% wameondoka bado 50%



Hii ngoma ngumu lakini itaisha kabla Kesi




Gigi akachokaa akahamaki hajui ashukuru au amtunuku Marion kimwili au!



Maana kazi za kuweka kichwa kwwenye sahani sio zake kabisa, akahisi ameingia choo cha kiume


Bonge akakamatwa na watu asiowajua, wakamfunga macho, mikono, miguu wakampiga weee afu wakamtupa kwenye shimo reeeefu Bonge akashtukaaaa kuangalia saa saa 11 asbh kumbe alikuwa anaota akainuka kumwangalia mtoto wake amelala shwari, mume hayupoo dah akachoka akawa amekaa tu kitandani anawaza na kuwazua hajui ndoto ina maana gan, akaamua kumpandia hewani Matusi hapatikani

Akampandia mfuasi wake hapatikani, akampigia his right hand man hapatikani mmmh asbh ikawa ngumu

Akaamua kujiandaa hata job hakwendaa akaenda kumcheki Matusi, kufika nyumbani mwake kufungua ni madamu kibaooo watu wamekufa kiroho mbayaaa, hapo saa 12 asbh, akasogea kuangalia akakutana na kichwa cha Matusi kimekatwa, chini kuna karatasi imeandikwa you are next

Akakimbia mpaka kurudi home saa 1 asbh, akamwelezea maza yake, maza akaanza kuingia na wasiwasi akasema ngoja nimwulize mtu, kumpandia hewan big poppa che hapatikani wala nene,
Akampandia hewan msaidizi wake akamwambia ametekwa nyara hata wao wanamtafuta ila wanahisi kafichwa mikoani mistuni, mama bonge akachokaaa, akiangalia imevakia wiki 1 kuitwa mahakamani,

Mama Bonge: hajakuachia mzigo wangu wowote kabla hajapatwa na majanga?!

Msaidizi: ndio hata sisi twashangaa hata zile evidence zote zimepotea hazipo nadhan wamezichukuaa wale waliomteka Big Poppa yani mama hapa tumechanganyikiwa hatuelewi

Mama Bonge: kwani nyie hamna maadui zenu ambao mnahisi labda wanachukiana na Big Poppa

Msaidizi: tunae, anaitwa Matusi, sasa tumeenda kumcheki
Tumekuta keshauawa na kichwa kakatwa chini kuna karatasi imeandikwa you are next tukaondoka tusijekutwa na polisi hapo

Mama bonge akakosa pozi sasa maana hajui cha kufanya hajui afanyaje yani ni sheedah akakata simu akaendelea kuonge ana Bonge wanapanga juu ya usalama wao kesi wiki ijayo usalama wao mbovu hawajui cha kufanya dah hii ngoma ngumu

Wakiww wanaendelea kuumiza kichwa Mama Bonge akamkumbuka yule baba aliekuwa anampigia simu anamwimbia ila kwa namba ya private no

Akaenda tigo na voda kuulizia hawana msaada akaenda polisi kulalamika wakamwambia hii namba mbona haipo hewan ila ilikuwa inamilikiwa na babu mmoja akamtajaaa mama bonge akamkumbuka, akauliza kama anaweza pata current no yake, polisi wakamsaidia, kuna lingine au unataka tumkamate?!

Mama bonge: ngoja kwanza nitarudi afande ngoja niongee nae kwanza alafu ntakupigia kama mwingie kazini au la mama bonge akaondoka kufika job kazi haziendi akamwibukia hewani yule babu mzee akapokea

Mama bonge: eh vepee baba za masiku?!

Babu Mzee: salama, nani mwenzangu?!

Mama bonge: me fulani bin fulan

Babu mzee akaganda kama sekunde 5 akamwuliza enhe unataka nini kwangu?!

Mama bonge: nataka tuongee, napenda nikurudishe kazini najua haukuondoka vizuri, tafadhali naomba tuongee

Babu mzee: wapi tuongee sasa?!

Mama bonge: naomba tukutane sehemu flan, leo saa 10 jioni

Babu Mzee: sina nauli mama labda unifadhili

Mama bonge: ntakurushia elfu 30 uchukue taxi hapo uje fasta sawa

Babu Mzee: sawa mama asante, simu ikakatwaaa

Babu Mzee akampandia hewani
Gigi, mama nimepigiwa simu na mama bonge anataka kuongea na mimi
Keshatuma na hela hapa naona imeingia anataka kunirudisha kazini, niende au?!

Gigi: ulienda atakumaliza, ichukue hio hela we panda boat njoo pemba fanya fasta kabla hajakuletea watu kukumaliza

Babu Mzee: sawa mama akakata simu, akawa anakusanya kila chake, aondoke,ila anatoka tu mapolisi hao
Babu mzee upo chini ya ulinzi kwa kosa la kutishia amani ya mama bonge
Babu wa watu kawekwa pingu polisi moja

Saa 8 mama bonge akatia timu polisi, kumcheki mfanya kazi wake wa zamani anamwuliza me nawewe tumekoseana nini na tumekosana wap mpaka kuniletea majambazi nyumbani kwangu

Babu Mzee: me sina jambazi niliemleta mbonaa, unanisingizia embu liambie jeshi la polisi ukweli mama acha kuniweka kwenye wakati mgumu... babu kajitetea pale na nene lakini wapi

Huko Pemba nako Gigi akawa amepata wasiwasi akamweleza Marion, kuhusu yule Babu mzee me nahisi kuna kitu kibaya kinaendelea pale

Marion akampandia hewani ofisa wake, vepee natmatuta mtu anaitwa flan flan,

Ofisa: tunae ameletwa leo anashtakiwa na mama mmoja kibopa

Marion: ana kosa gan na dhaman gan?!

Ofisa: ana koss la kutishia amani ya huyu mama na dhamana yake dau mil 5, huyu ataozea jela

Marion: nikitoa mil 5.5 unaweza mtoa?!

Ofisa: sawa hamba shida mkuu

Simu ikakatwa

Marion akatuma kijaja wake amalipia dhamana, saa 10 dhamana akapewa akaondoka kijana wa Marion na Mzee mpaka Pemba, babu mzee anashangaa kitu kama movie vile

Kufika Pemba anashangaa anapokelewa na Gigi, he mama upo huku?
Umefikaje?!

Gigi: long story usijali, ilimradi upo salama hamna neno! Wakaingia ndani kupiga story, usiku wakala, wakanywa, wakacheka, wakachezaa wakalala

Asbh kukakucha, mama bonge akaamkia polisi saa 4 asbh, kufika anaambiwa mtu wako ametoka kwa dhamana ya mil 5.5 na mtu asiejulikana katuma kijana wake akamtoaa
Sie tumepokea maana dhamana uliweka wewe sio sisi

Mama bonge akachokaaa, dah! Nani huyu mshenz anafanya hivi jamaa! Akachoka akaamua kukaa chini kabisa sakafuni, machozi yanamtoka, kichwa kinamwuuumaaa

Ukiona mtu mzima analia, ujue kuna jambooooo!

MWISHO

About THE STORY BOOK

0 Comments:

Post a Comment